Na Shushu Joel, Dar.
Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi Geofrey Mkinga ameeleza mikakati ya uboreshaji wamiundombinu ya Barabara katika jiji hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi yake Mha. Mkinga alisema kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hasaan imezidi kuboresha miundombinu ya barabara katika Jiji la Dar es Salaam kwa lengo la kuondoa changamoto za ubovu wa miundombinu hiyo.
Aidha Meneja huyo wa TARURA Mkoa huo aliongeza kuwa kuboreshwa kwa miundombinu hiyo kunakwenda kutatua changamoto za foreni kwani tumeamua kuboresha barabara mbalimbali kwa kusudi la kuhakikisha barabara zinapitika.
" Tunaipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi ili kuendelea kuboresha barabara za Dar es Salaam" amesema Meneja wa TARURA Mha. Mkinga
Pia Meneja Mha.Mkinga amesema kuwa ni vyema kila mkazi wa Dar es Salaam kuhakikisha anakuwa mlinzi wa miundombinu ili iweze kutumika kwa vizazi vijavyo.
Naye Mwajuma Ally Mkazi wa Kitunda ameipongeza TARURA kwa kjendelea kuboresha miundombinu ya Barabara katika Mkoa wa Dar es Salaam kwani uwepo wa miundombinu yenye kupitika ni sawa na kukuza uchumi kwa wananchi kwani usafiri wa uhakika ni tiba ya usafirishaji wa bidhaa.
Aidha amewataka wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kuwa walinzi wa miradi inayotekelezwa na serikali kwa gharama kubwa.

0 Comments