SHULE YA FILBERT BAYI IMETOA ZAWADI KWA WAWAKILISHI WAO UMISSETA

Shule ya Sekondari ya Filbert Bayi imetoa zawadi ya fedha taslimu kwa timu ya riadha ya shule hiyo iliyofanya vizuri kwenye mashindano ya Umoja wa Michezo Shule za Sekondari  (UMISSETA) Taifa iliyomalizika hivi karibuni Mkoani Iringa.

Akikabidhi fedha hizo kwa wanamichezo tisa shuleni hapo, Ofisa Elimu Mkoa wa Pwani Jimmy Nkwamu amesema kuwa kutokana na ushindi wa timu hiyo kumeufanya Mkoa huo kuwa washindi wa kwanza wa mchezo huo kitaifa na wanne kwa michezo yote.

Nkwamu amesema kuwa kilichofanya timu ya riadha kuwa ya kwanza ni maandalizi yaliyofanywa na Mkoa ambapo iliweka kambi ya muda mrefu pamoja na motisha iliyokuwa ikitolewa kila timu inapofanya vizuri pamoja na ushirikiano na mshikamano uliokuwepo baina ya viongozi wa Mkoa na wachezaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi za Filbert Bayi amesema kuwa lengo la kutoa zawadi hizo za fedha taslimu ni kuwahamasisha wachezaji waliofanya vyema ni kuwapa hamasa ili waendeleze vipaji na vipawa vyao kwenye mchezo huo.

Bayi amesema kuwa walitenga fedha kwa kila mshindi kwa mchezo huo kwa mbio zozote kiasi cha shilingi 50,000 kwa atakayeshinda medali ya dhahabu, fedha shilingi 30,000 na shaba ni shilingi 20,000 ambapo Sharifa Rashid amepata dhahabu tatu.

Naye Ofisa michezo wa Mkoa wa Pwani Grace Bureta amesema kuwa shule hiyo ni moja ya shule ambazo zimekuwa zikiufanya Mkoa huo kufanya vizuri kwenye michezo ya shule za sekondari nchini UMISSETA kwani ina mazingira mazuri ya kuwaandaa wachezaji.

Wachezaji wengine waliotunukiwa ni Wiliam Makaranga dhahabu moja, Samwel Samwel shaba moja , Emanuel Dotto fedha mbili, Salma Samwel fedha moja huku wengine wakishinda kwenye mbio za kupokezana vijiti ambao ni Kimana Sitta, Zainab Seleman, Lucia Nestor, Enos Manengelo ambapo Meshack Emanuel akishika nafasi ya tano kurusha kisahani na Rashid Mtindaji alikuwa wanne kuruka chini.

Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Bodi ya  Taasisi ya Filbert Bayi Filbert Bayi Kushoto  akiwa na Ofisa Elimu Mkoa wa Pwani Jimmy Nkwamu.

Post a Comment

0 Comments