IVO MAPUNDA ATANGAZWA KUWA KOCHA MKUU TEMBO WORRIORS


 Na Mwandishi Wetu

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu kwa watu wenye ulemavu (TAFF) limetangaza Ivo Mapunda kuwa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ‘Tembo Warriors’. 

Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Ufundi wa Taff, Shaban Msangi amesema atakuwa kocha kwa muda wa mwaka mmoja huku akitazamwa mafanikio yake.

Msangi alisema kutokana na Tembo Warriors kukabiliwa na michuano ya Afrika Mashariki na Kati (CECAAF) inayotarajiwa kufanyika Septemba mwaka huu Bujumbura, Burundi Jumatatu watakutana na Ivo Mapunda kupanga siku ya kutangaza kikosi cha timu ya Taifa.

Ivo Mapunda ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba, Yanga pamoja na timu ya Taifa ya soka ‘Taifa Stars’ alikuwa sehemu ya benchi la Tembo Warriors mwaka 2022 kama kocha wa magolikipa katika michuano ya Kombe la Dunia yaliyofanyika nchini Uturuki.

Post a Comment

0 Comments