Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya siku moja Mkoani Pwani Julai 31,2025 ambayo ni mahsusi kwa ajili ya kuzindua bandari kavu ya Kwala iliyopo Halmashauri ya Kibaha Vijijini Mkoani Pwani.
Sambamba na uzinduzi wa bandari kavu pia Rais Dkt. Samia atazindua Kongani ya viwanda ya Kwala.
Yamebainishwa hayo leo tarehe 07, Julai na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge wakatai akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari Mkoani hapa na vyombo mbalimbali vya habari katika mkutano uliofanyika ofisini kwake Manispaa ya Kibaha.
"Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan atafanya ziara katika eneo la Kwala sehemu ambayo serikali imefanya uwekezaji mkubwa ikiwa pamoja na ujenzi wa viwanda vikubwa zaidi ya 250" amesema RC Kunenge.
Aidha Mheshimiwa Rais akiwa katika eneo la Kwala pia atazindua rasmi safari ya treni ya Mwendokasi (SGR) ya kubeba Makasha kutoka Dar es Salaam na kupeleka Dodoma.
" Bandari Kavu ya Kwala ina uwezo wa kuhudumia makasha 823 kwa siku na Makasha 30,000 kwa mwaka.
Kunenge amesema bandari kavu ya Kwala itaongeza ufanisi wa bandari ya Dar es Salaam ambapo kimsingi bandari hiyo inayokwenda kuzinduliwa Jukai 31 imelenga kusaidia kupunguza msongamano wa makasha katika bandari ya Dar es Salaam kwa asilimia 30.
RC amesema kuwa Dkt. Rais Samia wiku hiyo atazindua maeneo ya ujenzi wa bandari kavu kwa ajili ya nchi za DRC Kongo, Zambia,Burundi,Malawi, Zimbabwe na Uganda ambapo pia amesema kuwa nchi za Sudan na Somalia nao wameonyesha nia ya kujenga bandari kavu katika eneo hilo.
Wakati huohuo Rais Dkt. Samia atapokea mabehewa 160 ya reli ya kati ambapo kati ya hayo mabehewa 20 yamekarabatiwa na mabehewa 100 yamenunuliwa mapya na serikali na mengine 40 yamekarabatiwa na Shirika la Chakula Duniani pamoja na Wakala wa Ushoroba wa Kati.
Kunenge amesema kuwa Rais Dkt.Samia ataweka jiwe la msingi kwenye Kongani ya Viwanda ya Kwala yenye viwanda 250 Kongani ambayo ni kubwa katika nchi ya Tanzania.


0 Comments