Multichoice Tanzania kuwapa wateja nafasi ya “Kuonja Utamu wa Mitanange ya FIFA” kwa Kifurushi cha POA
Kampeni hiyo imezinduliwa leo Jijini Dar es Salaam tarehe 16, 2025 ambapo Kampuni ya Multichoice Tanzania, kupitia huduma yake ya DStv, imethibitisha dhamira yake ya kuendelea kuwa karibu na wateja wake kwa kuzindua kampeni mpya inayojulikana kama "Onja Utamu wa Mitanange", ikilenga kuwawezesha wateja kushuhudia michuano mikubwa ya FIFA kwa bei nafuu.
Akizungumza mapema leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Masoko wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo, amesema kampeni hiyo inalenga kutoa fursa kwa kila Mtanzania, hasa wapenzi wa michezo, kupata uhondo wa michuano hiyo mikubwa duniani 'LIVE' itakayopatikana kwa kupitia kifurushi cha bei ya chini kabisa cha POA.
“Tunatambua umuhimu wa burudani ya michezo kwa wateja wetu. Kupitia kampeni ya 'Onja Utamu', sasa mteja yeyote akilipia kuanzia kifurushi cha POA, atapata nafasi ya kujionea mechi zote za michuano ya FIFA moja kwa moja, bila kulazimika kubadilisha kifurushi,” amesema Shelukindo.
Amesema kuwa lengo kuu ni kuhakikisha hakuna Mtanzania anayekosa kushuhudia burudani hiyo ya kipekee, huku amesisitiza kwa kusema kuwa Multichoice Tanzania itaendelea kuwekeza katika kuhakikisha itatoa huduma bora na zenye thamani kwa wateja wake na zinapatikana kwa kila mtu bila kujali uwezo wa kifedha.
Kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa Thamani kwa wateja DSTV Irene Mwakijangala na Mkuu wa Masoko Multichoice Tanzania Ronald Shelukindo.Kampeni ya “Onja Utamu wa Mitanange” inakuja wakati ambapo mashabiki wa soka duniani kote wakiwa na hamasa kubwa kuelekea michuano hiyo mikubwa ya FIFA, na hivyo kuwa fursa adhimu kwa familia, marafiki na majirani kukusanyika pamoja na kufurahia burudani kupitia DStv.




0 Comments