HAJI JANGUO ACHUKUA FOMU JIMBO LA KISARAWE MKOANI PWANI

Katika mwendelezo wa vijana waliokuzwa katika malezi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na  kuonesha nia ya kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu ujao  Haji Janguo leo  tarehe 29 Juni 2025 amejiunga rasmi kwenye orodha hiyo kwa kuchukua fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Kisarawe kwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Janguo amechukua fomu na kukabidhiwa na  Katibu wa CCM Wilaya ya Kisarawe  Bi. Josephine Mwanga.

Kwa mujibu wa Janguo amesema kuwa  uamuzi wake unatokana na wito wa kuwatumikia wananchi wa Kisarawe kwa uadilifu, uwazi na maono mapya, huku akiahidi kutetea maslahi ya vijana, wanawake na wakulima wa Kisarawe.

Kisarawe inazidi kushuhudia hamasa ya kisiasa ikipanda, huku kada wengine kadhaa wakiwa tayari wameshachukua fomu katika siku za karibuni ishara ya ushindani wa hali ya juu ndani ya demokrasia ya CCM.

Haji Janguo .

Post a Comment

0 Comments