DAKTARI BINGWA WA USINGIZI MUHIMBILI ZHANG JUNQIAO AFARIKI DUNIA


Na Malisa GJ

Tumempoteza daktari Bingwa wa dawa za usingizi Hospitali ya Taifa Muhimbili. Dkt.Zhang Junqiao (38) amefariki juzi tarehe 15 Juni 2025 huko  Kigamboni Jijini Dar  es  Salaam baada ya kuzama majini wakati akimuokoa mwananchi aliyekuwa anazama. Siku ya tukio Dkt.Zhang alimuona mwananchi akizama na yeye kuamua kujitosa majini kumuokoa. 

Alipomfikia alimpatia jaketi lake la kuogelea na yeye kwa kuwa ni mzoefu akaogelea bila jaketi. Raia aliyekua akizama alifanikiwa kuokolewa, lakini maji yalimzidi nguvu Dkt.Zhang akazama na kupoteza maisha.

Dkt.Zhang alikuwa daktari Bingwa wa Dawa za Usingizi na Ganzi (Anesthesiologist), raia wa China aliyekuwa anafanya kazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Dkt.Zhang alikua na shahada ya udaktari wa binadamu (Bachelor of Medicine) Shahada ya upasuaji (Bachelor of Surgery), shahada ya umahiri katika matibabu ya ndani (Master of Internal Medicine) na shahada ya umahiri katika dawa za usingizi (Master of anesthesiology). Pia alikua na cheti cha ithibati ya kimataifa cha kuhudumu kama daktari bingwa wa dawa za usingizi katika nchi zaidi ya 100 duniani (NMLE).

Dkt. Zhang atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa wa kuhudumia jamii ya watanzania, pamoja na umahiri wake kufundisha njia mpya za dawa za usingizi na ganzi. Atakumbukwa pia kwa ucheshi wake, uchangamfu wake na passion yake katika kazi. 

Dkt. Zhang amekufa kishujaa akijaribu kuokoa maisha ya Mtanzania mwenzetu aliyekua akizama. 

 Binti yake alimuona mwanamke wa kitanzania akitapata baada ya kuzama majini wakati anaogolea kisha akamwambia baba yake. Baba yake alijitosa kwenda kumwokoa mwanamke huyo.

 Muhimbili. Dkt. Zhang ameacha mjane na watoto wawili wa kike. 

Wapili kutoka kushoto  ni mke wa Dkt.  Zhang akilia  kwa uchungu mara baada ya kuwasili nchini   kushiriki mazishi ya mume wake

ambapo mwili wake utachomwa moto siku ya Ijumaa Jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments