Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uteuzi alioufanya leo June 23 2025, amemteua Mkuu wa zamani wa Jeshi la Polisi Tanzania Balozi Simon Nyankoro Sirro kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
Balozi Simon Sirro ni miongoni mwa Wakuu wapya wa Mikoa watano ambao wameteuliwa leo June 23 2025 ambapo wengine ni Kheri Dennis James aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Iringa, Mboni Mhita aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Beno Malisa aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Mbeya na Jabir Makame aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe.

0 Comments