WAZIRI MASAUNI ZIARANI OSLO NORWAY

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  Muungano na Mazingira Mhe.Hamad Masauni ameongoza ujumbe wa Tanzania  kutembelea Kampuni ya Hafslund Celsion inayojishughulisha  na ukusanyaji na  kutengenisha  taka katika Manispaa ya  Oslo nchini Norway. 

 Katika Ziara Hiyo Mhe Masauni ameambatana  na Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Tone Tinnes  pamoja na Maafisa kutoka Ubalozi wa Norway nchini Tanzania. 

Katika Ziara hiyo Ujumbe wa Tanzania umepata fursa ya kujionea jinsi Kampuni hiyo inavyotumia mbinu mbalimbali za ukusanyaji wa taka na  jinsi  inavyotenganisha taka na kuzalisha bidhaa mbalimbali ikiwa pamoja na kuzalisha  umme.

Jiji la Oslo lina wakazi wapatao 725,000 ambapo kulingana na taarifa ya  mwaka 2023 kila mkazi huzalisha takribani kilo 157 za taka kwa mwaka.

 Kampuni ya Hafslund ilianza kazi ya utenganishaji taka mwaka 2012 ili kuhamasisha utenganishaji wa taka Kampuni hiyo imekuwa ikitoa bure mifuko ya aina tatu ya kuhifadhia taka ambapo mfuko wa kijani umekuwa ukitumika kwa ajili ya taka za aina ya vyakula na  mfuko wa zambarau taka za plastick   taka zinginezo huhifadhiwa katika mfuko wa rangi nyeupe.

 Akielezea jinsi Taasisi hiyo inavyofanya kazi Mshauri wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Bw. Mads  Danielsen amesema kwamba Taasisi hiyo ina matawi matano ambayo yanajihusisha na upokeaji wa taka zitokanazo na mimea, vigae,vyuma chakavu, samani zilizovunjika na magodoro taka hizi hujulikana kama taka zenye ujazo mwingi 

(Bulky Waste).

 Taka zingine ni taka hatarishi zitokanazo na vifaa vya umeme na taka zinazoweza kurejelezwa kwa matumizi mengine ili kuhakikisha kuwa wananchi wa Jiji la Oslo wanatenganisha taka bila shurti Bw. Danielsen amemueleza Mhe. Masauni na ujumbe wake kuwa wamekuwa wakitumia njia mbalimbali kuelimisha umma ikiwa ni pamoja na sinema, redio,magazeti, vipeperushi , watu maarufu, mabango, matangazo kwenye vyombo vya usafiri, mitandao ya kijamii, muongozo wa kutenganisha taka, maonesho na shughuli mbalimbali za uhamasihaji.

Utenganishaji huo wa taka umeiwezesha Kampuni ya Hafslund kuanzisha baadhi ya biashara kama  uzalishaji maji yanayotokana na Mvuke unazalishwa baada ya kuunguza  taka, biashara ya umeme, biashara ya  kaboni uzalishaji wa mbolea na uuzaji wa vitu na vifaa vilivyotupwa ambavyo vinaweza kutumiwa na watu wengine. 

Aidha baada ya mkutano huo ujumbe wa Tanzania umetembelea kiwanda hicho na kujionea hatua mbalimbali za kutenganisha  taka.

 Kama nchi zingine duniani Tanzania nayo inazalisha taka hivyo kutekutenganisha  taka hutoa fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuzaliza bidhaa zingine zenye manufaa na kuzalisha ajira.

Post a Comment

0 Comments