JAB YATOA ONYO KWA WAANDISHI WATAKAO GHUSHI VYETI

Mwenyekiti wa Bodi ya  Ithibati  (JAB) Tido Mhando 

Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), imesema waandishi wa habari ambao wataghushi vyeti na kuvitumia katika mfumo mpya wa kidigitali wakigundulika watachukuliwa hatua hali za kisheria ikiwa ni pamoja na kufunguliwa kesi ya jina na kufungiwa.

Mwenyeti wa JAB Tido Mhando amesema  hayo leo  tarehe 19 Mei 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za JAB zilizopo Jijini Dar es Salaam na kusema mfumo wa JAB ambao unajulikana kama TAI-HABARI una uwezo wa kubaini vyeti feki hivyo ni vema mwandishi kabla hajaweka cheti chake ajiridhidhe kwanza kwa kukihakiki.

"Tumepata taarifa kuwa kuna vyuo vinatumika kutoa vyeti vya kughushi  na wote watakaofanya hivyo kwa uchu wa kupata fedha nasema wazi kuwa tutakuwa wakali kwani tutafuatilia taarifa zako katika mamlaka husika hata kama mmeanza kujipitisha kwenye vyuo hivyo  ndani ya miezi miwili ili kuhalalisha kununua vyeti vya kitaaluma tutawabaini kwa njia tutakazo zitumia sisi", amesema, Mhando.

Mhando amesema waombaji lazima wazingatie vyeti ni halali na vimehakikiwa na mamlaka husika,ikwa pamoja na TCU na NACTVET mamlaka hizo ndizo zitatoa    taarifa  sahihi ili kuepusha usumbufu  ,pia picha ya  muombaji na taarifa zake ziwe za karibuni", amesema

Kwa mujibu wa kanuni ya 17(a) ya kanuni  za sheria  ya huduma  za habari watu wanaopaswa  kujisajili  ili  kuthibitishwa na kupatiwa  vitambulisho ni wahariri,waandishi wa kujitegemea,watangazaji, wapigapicha wa vipindi vya habari, wanafunzi wa  vyuo vya uandishi wa habari wanaokwenda mafunzo kwa vitendo na waandishi wa habari wa kigeni.

"Ili kujisajili katika mfumo wa TAI -HABARI mwombaji anatakiwa na namba ya simu na barua pepe vinavyofanya kazi ,picha ndogo ambayo haijaskaniwa, vyeti vya elimu  vilivyo sainiwa, barua ya utambulisho kutoka katika taasisi anayotoka au anakopeleka kazi zake ikiwa ni mwandishi wa kujitegemea atahitajika kutuma nakala ya kitambulisho chake cha taifa  NIDA na ada  ya JAB ni 50,000 na Dola 500 kwa wandishi kutoka nje ya nchi ambayo itadumu kwa muda wa miaka miwili", amesema.

Mhando amesisitiza kuwa mahitaji haya ni muhimu ili kukamilisha  mchakato  wa maombi kwa mafanikio.

Amesema waaandishi wanapaswa kuingia kwenye kiunganishicha https//taihabari.jab.go.tz na kufuata maelekezo ya kujisajili.

Mhando amesema kuwa  baada ya  kujaza  taarifa  kwa usahihi mwombaji atapokea neno siri (code) kupitia SMS na  barua pepe ili kuendelea na hatua za kujaza wasifu, kufanya maombi,kupata ankara ya malipo, kulipia na  kuwasilisha maombi ya kupata  kitambulisho (Press Card).

Mhando amesema kitambulisho cha Bodi (Press Card) kitatumika mahali popote ambapokutakua na shughuli  za kihabari  zinafanyika  na mahali popote ambapo mwandishi wa habari  anataka kufanya kazi ya kutafuta  habari  isipokuwa  maeneo  maalum  yaliyozuiliwa kisheria.

Bodi ya Ithibati JAB ilizinduliwa Machi 3, 2025 na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Prof.Palamagamba Kabudi Jijini Dar es Salaam.

Wakati huo huo Mhando amesema kuwa JAB inamipango endelevu kwa wandishi wa habari kwa sababu watakua na mfuko wa mafunzo ambao utakua na lengo la kuwaendeleza kitaaluma na kuwajengea uwezo,  kukuza maudhui pia wamejipanga kuanzisha kituo ambacho kitakua huru na rafiki kwa waandishi wa habari watakaokuwa wanachama wa JAB ikiwa ni pamoja kuwakutanisha na kubadilishana mawazo sambamba na kufanya kazi zao.

Amesisitiza kua JAB ni mwamvuli wa kutetea haki za wanahabari pale watakapokumbana na changamoto  katika kazi zao za kila siku kuwalinda na vitisho  na manyanyaso yatakayojitokeza wakiwa kazini.

Post a Comment

0 Comments