NMB WACHANGIA SHULE NA ZAHANATI MKURANGA

Benki ya NMB imeungana na kusherehekea  pamoja katika kilele cha siku ya Wanawake Duniani  kwa kutoa michango ya madawati  100 na vitanda20 kwa Shule  na mabati 100 kwa ajili ya kuezeka Zahanati  Wilayani Mkuranga. 

Akikabidhi  Madiwati kwa Mkuu wa Wilaya Mkuranga  Meneja wa Kanda   Dar  es Salaam  na Pwani  Seka Urio amemkabidhi  Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga  Khadija Nasri madawati 100 ambapo madawati 50 yatapelekwa Shule ya Kisemvule  ,madawati 25 Shuke  ya Msingi Chatembo na madawati mengine 25 yatapelekwa Shule Msingi  Chatembo.

 "Tunayoheshima  kubwa  sana kushiriki  kwenye maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Wanawake  2025" amesema Urio.

Makabidhiano  hayo yamefanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kisemvule tarehe 8 Machi 2025 ambako ndiko kumefanyika maadhimisho ya  sherehe hizo kimkoa.

Akizungumza  kwa niaba  Mkuu wa Mkoa wa Pani Alhaji Abubakari Kunenge, Mbunge wa Viti Maalum Chama Cha Mapinduzi (CCM),

Mh.Subira Mgalu amewaeleza wanawake waliofika kwenye sherehe hizo kuhakikisha ifikapo wakati wa uchaguzi mkuu wa 2025 wanamchagua tena Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan  kwa awamu nyingine tena.

"Twendeni tukampe kura za ndiyo kwa sababu hakuna mtu yeyote mwenye uwezo wa kuzuia uchaguzi mkuu hilo liko wazi"

amesema Mgalu.

Sherehe hizo zimepambwa na wahudhuriaji kutoka Taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na TAKUKURU, PSSSF, NMB,CRDB, JKT RUVU, Mtandao wa Askari  wa Jeshi la Polisi  Pwani Shirika la Elimu Kibaha, Nyumbu,Wajasiriamali  wote ndani ya Mkoa wa Pwani ambao walipata fursa ya kunesha bidhaa zao na wengineo wengi.


Post a Comment

0 Comments