MAKAMU WA RAIS DKT. PHILIP MPANGO KUZINDUA MWENGE WA UHURU PWANI

Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Isidory Mpango atazindua  mbio za Mwenge wa Uhuru  tarehe 2 Aprili 2025.

Akizungumza  leo  tarehe 26 Machi 2025  kwenye mkutano na Waandishi wa Habari  Waziri  wa  Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Ridhiwani  Kikwetete (MB) alipozungumza  kwenye Ukumbi wa Mikutano  wa Ofisi  ya Mkuu wa Mkoa  Pwani.

"Awali ya yoye  napenda  kutumia fursa  hii kumshkuru Mungu kwa kurukutanisha  siku ya leo  tunapoelekea katika  tukio la uzinduzi  wa Mbio za  Mwenge wa Uhuru  kwa mwaka 2025" amesema Kikwete.

"Napenda  kutoa   taarifa kwa umma  kuwa  uzinduzi  wa Mbio za Mwenge  wa Uhuru  utakuwa katika Uwanja  wa Shirika la  Elimu Kibaha, Mkoani Pwani" amesema  Kikwete.

Waziri Kikwete  ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mkoani  Pwani amesema kuwa  baada ya Mbio za Mwenge  wa Uhuru kwa mwaka 2025 kuzinduliwa Mhe.Dkt.Philip Isdor Mpango  atawakabidhi  vijana  sita waliochaguliwa kutoka Tanzania  Bara na Zanzibar,  watakaokuwa na jukumu la  kukimbiza  Mwenge wa Uhuru katika Mikoa 31 yenye jumla ya Halmashauri 195 za Jamhuri  ya Muungano wa  Tanza kwa siku 195 na katika kipindi  hicho chote,Mwenge wa  Uhuru  utafanya kazi ya kuhamasisha amani, umoja  upendo  na  mshikamano wa  Kitaifa .Vilevile  Mwenge wa Uhuru utawahimiza wananchi kushiriki.shughuli za maendeleo ya kijamii na kiuchumi  katika  maeneo yao ya Halmashauri. 

Kauli mbiu mwaka huu  umebeba  kaulimbniu  isemayo 'Jitokeze kushiriki uchaguzi Mkuu wa 

Mwaka 2025  kwa Amani na Utulivu 'ujumbe  wa Mwenge wa mwaka huu unalenga  kuwaelimisha na kuwaunganishs wananchi  wote  wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania  kushiriki kikamilifu  katika uchaguzi Mkuu

 kwa amani utakaofanyika mwaka huu.

Aidha Mwenge wa Uhuru  utatumika kuelimisha wananchi katika maeneo yote nchini juu ya masuala  ya kisekta na  katika muktadha wa  Kitaifa  na Kimataifa ikiwa ni pamoja  na maradhi  yanayotishia  ustawi  wa watu kama vile UKIMWI, Malaria na  kupambana  na  matumizi  ya Dawa za Kulevya na Vitendo vya rushwa .Vilevile  katika Halmashauri  zote  utakapokuwa Mwenge wa Uhuru  utaendelea  kuwaelimisha  wananchi juu ya umuhimu wa Lishe Bora  kwa afya imara.

Mwaka 1961  Hayati Mwalimu  Julius  Kambarage  Nyerere  aliuwasha   Mwenge wa Uhuru  na kumkabidhi Mwenge wa Uhuru  na Bendera ya Taifa

Luteni  Alexander  Ngweba Nyirenda  na kikosi cha vijana wenzake  wakaupandisha  Mwenge wa Uhuru  na Bendera  ya Taifa  la Tanganyika juu ya  Mlima  Kilimanjaro. Mwalimu Nyerere  wakati akitoa  hotuba  ya siku  ya Uhuru  aliwatangazia  Watanganyika , Afrika  na Dunia  kwa ujumla kwa  kutamka maneno haya"Sisi tumekwisha  uwasha  Mwenge wa Uhuru na kuuweka  juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike ndani na nje  ya mipaka yetu,ulete matumaini pale ambapo hakuna matumaini,ulete upendo mahali penye chuki na heshima mahali penye dharau" amesema  Mhe.Kikwete.

 "Watanzania wenzangu tunatambua kuwa falsafa hii ya Mwenge wa Uhuru, ndiyo chimbuko la Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964,Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa mwaka 1964 na Azimio la Arusha la mwaka 1967.Niwasisitize watanza tuendeleze Mwenge wa Uhu kama ulivyo asisiwa na Hayati Mwalimu Julius Kambarage mwaka 1961 wakati Taifa letu lilipopata Uhuru" amesema.

"Napenda kutoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Pwani,Mikoa ya jirani na watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi"amesema Mhe.Kikwete.

Post a Comment

0 Comments