MASHIRIKA YA UMMA ACHENI WATAKIWA KUJITEGEMEA

Ofisi ya Msajili wa Hazina pamoja na Ofisi ya Mkaguzi kuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imeunda kamati ya pamoja ya kuangalia namna mashirika ya umma yanavyoweza kujiendesha kwa faida na kuacha utegemezi wa Serikali.

Akizungumza na Waandishi wa habari Februari 26,2025 msajili wa hazina Nehemiah Mchechu amesema kuwa makubaliano hayo yamefikiwa baada ya kikao kazi cha  siku mbili kati ya ofisi ya hazina na ofisi ya Taifa ya mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG.)kilichoketi katika chuo cha uongozi cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Charles Kichere (kushoto) Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kikao kazi cha ofisi hizo kilichofanyika Februari 26 katika chuo cha uongozi cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kibaha Mkoani Pwani.

Mchechu ameongeza kuwa katika  muendelezo wa hilo walilolifanya kuna taasisi tatu ambapo kwa ujumla wake ndio taasisi mtambuka huku akitaja taasisi hizo kuwa ni ofisi ya CAG,Wizara ya Fedha pamoja na ofisi ya Utumishi wa Umma.

Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali, (CAG). CPA Charles Kichere amesema kuwa kikao kazi  hicho cha siku mbili kilikuwa pia na lengo la kupata michango ya wadau kwa ajili ya kuboresha mashirika ya Umma.

Post a Comment

0 Comments