MANGO MABINGWA JAFO CUP 2024-25

Mhe.Dkt.Selemani Jafo pia  ni Mbunge wa Jimbo la Kisarawe akizungumza na Waandishi wa Habari hawapo  pichani  alipokuwa mgeni rasmi kwenye  fainali ya Jafo Cup iliyochezwa  Manerumango Kisarawe Mkoani Pwani.
Zawadi za Pikipiki zilizotole kwa  mshindi wa kwanza  hadi wanne kwenye michuano ya Jafo Cup 
Dkt.Jafo akimvisha  medali mtoto wa mchezaji wa timu ya Mango ambao ndiyo mabingwa wa Jafo Cup.
Timu ya Tarafa ya Manerumango 'Mango' yenye Maskani yake Manerumango  Wilayani Kisarawe   wameibua kuwa mabingwa katika fainali ya michuano ya Jafo Cup iiyocheezwa tarehe  Februari  9 2025 baada ya kuwatoa timu ya Kisarawe  1-0 kwa njia ya  penati.

Kipute hicho kimechezwa kwenye Uwanja wa Manerumango  Kisarawe  Mkoani  Pwani  ambapo  timu ya Mango katika  kipindi cha kwanza dakika ya 12 waliifunga Kisarawe  na waliendelea kuongoza hadi walipokwenda  mapumziko. 
Katika kipindi cha pili  cha mtanange huo  ndipo timu ya Kisarawe  ikasawazisha goli  hilo na hadi dakika 90 za mechi hiyokumalizika hakukua  na mbabe  ndipo ikaamuliwa  kupigwe mikwaju mitano kwa kila timu pia   wote walitoka suluhu ya 4-4 ikaongezwa tena penati moja kwa kila timu   ndipo Mango wakawachapa Kisarawe 1-0 na kuibuka washindi wa Jafo Cup2024-25.
Kutokana na ushindi huo Mango wamekabidhiwa Kombe,kitita cha Mil.2 na pikipiki mbili zawadi  hizo wamekabidhiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara ,
ambaye pia  Mbunge wa Jimbo la Kisarawe Dkt.Selemani Jafo.

Timu ya Kisarawe wameshika  nafasi ya pili na  wamezawadiwa  kitita cha MI.1 na Pikipiki moja .

Mshindi wa tatu    ni timu ya Mzenga  na wanne ni Kurui.

Mbunge Dkt.Jafo amesema " Nikiwa Mbunge wa Jimbo la Kisarawe  na ndiye  niliyeandaa michuano hii nimefarijika sana na mwamko wa vijana na wananchi kwa namna  walivyojitokeza kucheza na kuehangilia na hii ni kwa mara ya kwanza ushindani umekuwa mkubwa kila mtu aliyefika uwanjani hapa ni shahidi  tumeimarisha udugu na umoja kwa wana Kisarawe" amesema Dkt. Jafo.
Timu zilizo ingia fainali wamepewa zawadi ambao ni Mango amepata 80,000    Kisarawe 70 , 000 na Mzenga na Kurui amepata kiasi cha 50,000  kila mmoja.

Michuano  ya Jafo ilianza kutimua vumbi Julai 2024 ilichezwa kuanzia ngazi ya vijiji katika Kata 17.
Wakati huohuo amewahamasisha wananchi wa  Kisarawe  kujitokeza kwa  wingi  kwenye zoezi  la kuboresha taarifa zao kwenye Daftari  la Kudumu la Mpigakura.
"Ninapenda kuwakumbusha  kuwa ni wajibu kwa kila mwananchi kwenda kujitokeza kuboresha  taarifa zake kwenye Daftari la Kudumu la Mpigakura ikiwa ni katika kuelelea uchaguzi  mkuu wa Rais Wabunge na  Madiwani hii ni kwa wote  waliotimiza  umri wa  miaka 18 na zaidi au watakaotimiza  umri huo  wakati au kabla  ya tarehe  ya Uchaguzi  Mkuu wa 2025 na ambao  hawajapoteza sifa kwa mujibu wa sheria
"amesema Dkt.Jafo .

Aidha zawadi zingine zimetolewa  kwa waamuzi 14  huku kila mmoja amepata kiasi cha .Sh.100,000  waalimu wa timu

Post a Comment

0 Comments