Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari akizungumza na Waandishi hawapo picha.
MKUU wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge ametoa wito kwa wakaazi wa Mkoa wa Pwani kujitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi wa kuwasha Mwenge Kitaifa utakaofanyika Aprili 2 ,2025 utakao washwa kwenye Viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha.
"Mtakumbuka kuwa wakati wa maadhimisho ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru, kumbukumbu ya Baba wa Taifa na wiki ya Vijana Kitaifa kilichofanyika Mkoani Mwanza Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliwatangazia wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2025 utafanyika katika Mkoa wa Pwani.
"Mkoa wa Pwani umepokea kwa heshima ya kuteuliwa kuwa mwenyeji wa shughuli ya uzinduzi wa mbio hizo unaotarajiwa kufanyika Aprili 2, 2025 katika Uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha" amesema RC Kunenge.
"Tunatarajia sherehe hizo zitahudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa, Mikoa ya jirani na Wilaya zote za Mkoa wetu pamoja na wananchi" amesema Kunenge.
Amesema hayo leo asubuhi alipozungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika uliofanyika ofisini kwake kwamba sherehe hizo zitapambwa na matukio mengi ikiwa ni pamoja na halaiki na burudani zingine kutoka kwa wasanii maarufu nchini" amesema.
Kaulimbiu ya mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 inasema 'Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa 2025 Kwa Utulivu na Amani' kauli mbiu hii inahimiza wananchi wote Kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi kwa utulivu,mshikamano na uzalendo ili kudumisha amani na maendeleo ya taifa letu na wakimbiza Mwenge wa Uhuru watatoa ujumbe unaoambatana na kaulimbiu hii.
"Hii ni fursa kubwa kwetu sote Wana Pwani kwani uzinduzi huu ni chachu ya maendeleo ya Mkoa wetu na hasa katika suala la kiuchumi kama vile huduma za malazi, chakula, usafiri, vinywaji , utalii na mengineyo mengi hivyo nitumie fursa hii kuwahamasisha na kuwaomba wananchi wote wa Mkoa wa Pwani na maeneo jirani kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uzinduzi huu"amesema RC Kunenge.
Mwenge wa Uhuru ni alama ya maendeeo, mshikamano na amani hivyo tushiriki kwa moyo mmoja katika tukio hili muhimu kwa taifa letu" amesema RC Kunenge.
Aidha amesema kuwa Mwenge wa Uhuru ni alama ya maendeleo , mshikamano na amani hivyo tushiriki kwa moyo mmoja katika tukio hili muhimu kwa taifa letu.
Baada ya uzinduzi huo Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika Halmashauri zote tisa za Mkoa wa Pwani ambapo utakagua na kutembelea na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

0 Comments