RENMIN NA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU NYERERE WASAINI MKATABA WA KUBADILISHANA WATAALAMU

Shule ya Uongozi  ya Mwalimu Nyerere imeingia makubaliano  kwa mara ya pili ya ushirikiano na Chuo Kikuu cha Renmin cha China  katika nyanja za mbalimbali zikiwemo za mafunzo utafiti na kubadilishana wataalamu.

Wakisaini makubaliano hayo kati ya Mkuu wa Shule ya Mwalimu Nyerere Profesa Marcellina Chijoriga na kiongozi Mkuu wa Chama Tawala Cha China Cha (CPC) kwenye chuo cha Renmin Zhang Donggang katika Shule hiyo iliyopo Kibaha Mkoani Pwani huku wakishuhudiwa na Wakufunzi wa Vyuo mbalimbali nchini na Wakufunzi wa Vyuo kutoka China.

Profesa Chijoriga amesema kuwa makubaliano hayo yatakuwa ni kwa ajili ya kubadilishana Wataalamu ambapo wao watakuja huku na wa Tanzania watakwenda kwao ikiwa ni sehemu ya kubadilishana uzoefu.
“Chuo hicho cha Renmin ni cha tatu kwa  ukubwa  na kikongwe  nchini China  na kiko vizuri kwenye masuala ya utafiti wa uandishi wa vitabu na katika masuala ya uandishi wa vitabu ambapo ushirikiano huo utakuwa na manufaa makubwa sana kwa pande zote mbili,”amesema Prof.Chijoriga.

Amesema kuwa Chuo hicho cha Renmin kinauwezo mkubwa wa kuwajengea uwezo Viongozi wa chama na serikali kwani kiko vizuri sana katika ufundishaji masuala hayo na watatumia uzoefu ili kujifunza kupitia kwao kwani kimeanza muda mrefu.
“Faida hiyo ni kwa vyama sita vya ukombozi Kusini mwa Afrika ambapo China ni msaidizi mzuri kwani wamesaidia ujenzi wa shule hiyo ambavyo ni CCM, FRELIMO, SWAPO, ANC na ZANU-PF msaada kutoka chama cha ukomunisti cha nchini China CPC” amesema .  
Aidha amesema kuwa chuo hicho kilichopo Beijing China kilianza ushirikiano mwaka jana ambapo Uongozi wa Shule walikwenda na katibu mkuu wa CCM wakati ule Daniel Chongolo na sasa wameanza safari mpya kwa kusaini mikataba hiyo kwani kina uzoefu mkubwa nani cha zamani sana.
“Tunashukuru sana kwani wametuonyesha ushirikiano mkubwa na makubaliano ya kutengeneza ushirikiano huu ni sasa safari mpya imeanza leo  na wametupa vitabu tunawashukuru kwani maktaba yetu sasa itakuwa na vitabu vingi na wasomaji wataweza kujifunza masuala mbalimbali ya nchi ya China,”amesema Prof.Chijoriga.
"Tumeingia  makubaliano  katika nyanja  za kubadilishana viongozi kwenda kuwa wakufunzi na kubadilishana uzoefu  katika mafunzo  yatakayofanyika kati nchi hizi mbili   tayari Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Palamagamba Kabudi  amekwenda China na  kutuwakilisha, amesema Prof. Chijoriga.

" Tutashirikiana  na China  katika nyanja za tafiti  mbalimbali  kwa sababu hawa wenzetu wako  mahiri zaidi kwenye tafiti mbalimbali" amesema   Prof.Chojoriga.

Kwa kupitia mkataba huu tumekubalia kuwa  tutawajengea uwezo viongozi wa chama  na serikali  pia ikumbukwe hii ni faida kwa vyama sita rafiki vya ukombozi Kusini mwa Bara la Afrika .
 
Aidha Prof.Chijoriga ametoa shukrani  kwa  serikali  ya China  kwa  kutoa  msaada wa maktaba Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius  Nyerere ambayo imewaongezea thamani  na kusema  kuwa wakati umefika  wa nchi navyama rafiki kujifunza kwa wenzetu.

 Dkt. Evaristo Haule Naibu Mkuu wa Chuo Mipango Fedha na Utawala Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere amesema kuwa China imefanikiwa na tumeona namna gani kutumia njia ili kuona wao wamefanyaje na kufikia hatua kubwa kiasi hicho kwenye maendeleo na CPC inavyotoa dira kuongoza nchi yao wanataka twende pamoja katika miradi yao mikubwa ya kidunia.
Dkt. Haule amesema ili kwenda pamoja hivi karibuni Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekwenda China kwenye mkutano wa ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika wao wana dira  na kufanya kazi kwa bidii na kuwa na nidhamu ya kazi na watu wawe na uzalendo wa nchi watu wanaangalia changamoto badala ya kuangalia fursa zilizopo.
Naye Dkt. Theresia Dominick kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam akizungumza kwa niaba ya Wakufunzi  wa Shule ya Mwalimu Julius Nyerere  amesema kuwa  kwa kupitia  wenzetu wachina tujifunze  kuwa na nidhamu  ya kufanya kazi kwa bidii,"mchina ana nidhamu ya juu katika utendaji wake wa kazi kadhalika  wanatabia  ya kuzingatia chakula  kwa sababu wanaamini  katika  kulinda afya zao  kwa kuzingatia faida ya chakula anachokula  kina faida gani ama kitamletea madhara gani tofauti na sisi ambao huwa tunakula tu ilimradi tumbo lijae"
Ameongeza  kwa kusema kuwa watanzania tunapaswa kuwa na nidhamu ya fedha kwa sababu wachina hawana tabia ya ufujaji wa fedha  hata kama anazo huwezi kumuona ama kumkuta anabadili mwenendo wa maisha yake" amesema Dkt.Theresia Dominic. 

Amesema  kuwa baadhi ya wafanyabiashara Watanzania wamekuwa wakienda China hivyo wanapaswa kujifunza tabia za Wachina za kufanya kazi kwa bidii na kuwa na nidhamu ya jambo kwani wanalolifanya Wachina duniani ni mfano wa kuigwa.
Naye kiongozi huyo Zhang Donggang amesema kuwa ushirikiano uliopo baina ya China na Tanzania na nchi nyingine ni katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo ambapo wao wanaangalia sana maslahi ya wananchi.
Donggang amesema kuwa nchi za Afrika na China zinapaswa kushikana mkono katika kuhakikisha zinapiga hatua katika masuala ya kimaendeleo ili kudumisha umoja uliopo kwani umoja uliopo umeleta mafanikio makubwa.
Kutoka kushoto  ni Naibu Mkuu wa  Chuo Cha  Kumbukumbu  ya Mwalimu Nyerere  Dkt. Evaristo Haule Shule ya Uongozi Mwalimu Nyerere Profesa Marcellina Chijoriga  na Mkuu wa Chama Tawala Cha China  Cha (CPC)kwenye Chuo cha Renmin Zhang Donggang wakiwa  katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini mkataba huo
Pro.Marcellina Chijoriga na Kiongozi Mkuu wa Chama tawala Cha China  ( CPC ) kwenye Chuo Cha Renmin Zhang Donggang wakitia saini ya makubaliano ya ushirikiano kati yao kwenye hafla fupi iliyofanyika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani 09,Oktoba ,2024.
Pro.Marcellina Chijoriga na Kiongozi Mkuu wa Chama tawala Cha China  ( CPC ) kwenye Chuo Cha Renmin Zhang Donggang wakiwa wameshika vitabu vyenye mikataba yao waliyosaini 09,Oktoba  2024  kwenye hafla fupi  iliyofanyika Shule ya Uongozi.
Pro.Marcellina Chijoriga na Kiongozi Mkuu wa Chama tawala Cha China  ( CPC ) kwenye Chuo Cha Renmin Zhang Donggang wakiwa kwenye semina fupi baada ya kusaini mkataba huo wa ushirikiano  kwenye hafla fupi iliyofanyika iShule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani  09,Oktoba ,2024 .

Post a Comment

0 Comments