OFISI YA WAZIRI MKUU, IBI ZASAINI MAKUBALIANO

Mtaalam wa Kujenga Uwezo kutoka Taasisi ya Mpango wa Biashara wa Kimataifa (IBI), Bi. Amtonga Amani akisaini makubaliano kati ya taasisi hiyo na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) kuhusu mashirikiano katika masuala ya Ufuatiliaji na Tathmini hafla iliyofanyika  katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma.
Picha ya pamoja mara baada ya kutia Saini makubaliano hayo ikiongozwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi na baadhi ya watendaji kutoka ofisi hiyo na Taasisi ya Mpango wa Biashara wa Kimataifa (IBI).
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Na Mwandishi wetu- Dodoma

Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu na Taasisi ya Mpango wa Biashara wa Kimataifa (IBI) zimesaini makubaliano kuhusu mashirikiano katika masuala ya Ufuatiliaji na Tathmini.

Makubaliano hayo yamesainiwa katika ukumbi wa ofisi hiyo ambapo mara baada ya kutia saini, Katibu Mkuu katika ofisi hiyo Dkt. Jim Yonazi amebainisha kuwa, lengo la kuanzisha mfumo wa tathmini na ufuatiliaji ikiwa ni kuhakikisha nchi inasonga mbele katika suala la tathimini na ufuatiliaji wa miradi yote ya serikali.

Dkt. Yonazi ameongeza kuwa ili kuweka mipango inayotekelezeka na kutoa matokeo chanya ipo haja ya vitengo vilivyoanzishwa kujengewa uwezo, jukumu ambalo huratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, huku akiwahimiza wadau wengine kuiunga mkono Serikali hatua iliyofanywa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) kwa kutoa ufadhili katika taasisi hiyo katika kuisaidia Serikali kwa kazi ya tathimini na ufuatiliaji.

“Tumeingia makubaliano na wadau kwa ajili ya kushirikiana katika kujenga uwezo wa ufuatiliaji na tathmini serikalini, ikiwa ni uamuzi wa serikali kuanzisha mfumo wa ufuatiliaji na vitengo katika serikali, hivyo ni lazima kujengewa uwezo jukumu ambalo limekabidhiwa katika Ofisi ya Waziri Mkuu la kufuatilia na kutathimini utendaji wa serikali nchi nzima,” alisema Dkt. Yonazi.

Aidha Dkt. Yonazi aliwahimiza wadau wengine wa maendeleo kujitokeza kuiunga mkono Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia kada ya ufuatiliaji na tathmini kuhakikisha shughuli za serikali zinafanyika na kuleta matokeo yanayokusudiwa.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akikabidhiana mkataba kati yake na Mtaalam wa Kujenga Uwezo kutoka Taasisi ya Mpango wa Biashara wa Kimataifa (IBI), Bi. Amtonga Amani, hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akisaini makubaliano kati ya ofisi hiyo na Taasisi ya Mpango wa Biashara wa Kimataifa (IBI) kuhusu mashirikiano katika masuala ya Ufuatiliaji na Tathimini, hafla hiyo imefanyika  katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma.

Post a Comment

0 Comments