LUTENI JENERALI SANYATWE WA JESHI LA ULINZI ZIMBABWE AMMWAGIA SIFA HAYATI MWL.J.K NYERERE

Kamanda wa Jeshi  la Ulinzi la  Zimbabwe Luteni Generali Anselem Nhamo Sanyatwe amesema Hayati Mwalimu Julius Nyerere atabaki kuwa Baba wa Afrika kwa sababu ameweza kuunganisha waafrika kwa kutumia lugha ya Kiswahili katika harakati za kupigania uhuru wa nchi zilizo katika Ukanda wa Kusini mwa Afrika.

Luteni Jenerali  Sanyatwe amesema  nchi ya Tanzania imekuwa mfano bora wa  kuigwa Barani Afrika  kutokana na  kuendelea kupokea wageni hasa wakimbizi kutoka katika nchi zao kama Congo, Msumbiji, Burundi, Rwanda, Zimbabwe na nchi zingine kutoka Afrika.

Ameongeza kwa kusema  kuwa  hivi sasa nchi ya Zimbabwe wameanza kufundisha Lugha ya Kiswahili Mashuleni, Vyuo Vya Elimu ya Juu nchini Zimbabwe kuna baadhi ya Watanzania ambao wamepata fursa ya kufundisha Lugha
ya Kiswahili.

kuendelea na ajira yake ya Ualimu ambayo ilikuwa na mshahara au ataendelea na harakati zake za kupigania Uhuru wa nchi yetu"amesema Dkt.Kikwete.

Akizungumzia umuhimu na sababu za kuanzishwa kwa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Dkt Kikwete amesema kuwa  lengo la kuwajengea uwezo wa kada mbalimbali za Uongozi kutoka Vyama sita rafiki ambayo ni CCM, FRELIMO, ANC, ZANU PF,  SWAPO na MPLA kwa ushirikiano wa Chama Cha kikomunisti Cha nchini China CPC.

Aidha amewataka Viongozi kuondoa dhana ya kwamba Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere ni ya Chama fulani bali ni ya Vyama vyote sita rafiki vya harakati za 
Ukombozi Kusini mwa Afrika.

Hatahivyo Rais Mstaafu Kikwete amesisitiza kuwa  Viongozi ambao wamepewa mamlaka ya kusimamia Shule ya Uongozi  kuendelea kuitunza miundombinu ya Shule hiyo na rasilimali zote za Shule zilizopo.

Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Prof. Marcellina Chijoriga amesema  katika salamu zake za ukaribisho kwamba Kongamano  hili limeandaliwa  kwa ajili ya kuenzi maisha ya Hayati Mwalimu Nyerere na pia kutumia fursa hiyo kujadili michango yake katika ukombozi wa Bara la Afrika.
Baadhi ya viongozi  wakimsikiliza  mgeni rasmi  ambaye pia alikua  ndiye msemaji mkuu kwenye  kongamano  hilo  Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete akiteta na Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Profesa Marcellina Chijoriga wakiteta jambo. 
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete  akipokea  zawadi ya shati kutoka kwa Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Profesa Marcellina Chijoriga
Rais  Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ndiye alikuwa msemaji mkuu wa Kongamano  hilo amesema  moja ya njia sahihi ya kumuenzi muasisi wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere ni kwa kutekeleza kwa vitendo aliyoyafanya wakati wa uhai wake kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali hususani katika Uongozi.

Ameyasema hayo   11,Oktoba 2024 wakati akifungua Kongamano la Maadhimisho ya kumuenzi Mwalimu Julius Nyerere chini ya kaulimbiu 'Mwalimu Nyerere na Vuguvugu la Ukombozi Tafakari Mshikamano, Uongozi, Pan-Africanism na Umoja wa Afrika", iliyofanyika katika Shule ya Uongozi ya  Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
National Congress (ANC- Afrika Kusini) SWAPO (Namibia), FRELIMO (Msumbiji), ZANU PF (Zimbabwe),  MPLA  (Namibia  ) na 
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwakilishi wa Chama Cha Kikomunisti  Cha China (CPC) Mabalozi, Wakuu wa Taasisi za Serikali, Mashirika yasiyo ya Kiserikali na wakazi wa Kibaha.
Kamati ya Ulinzi na Usalama wakitoa heshima kwa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete  wakati  akiingia kwenye Ukumbi wa mikutano wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani
Mhe.Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete akizungumza kwenye Kongamano la kumbukizi ya miaka 25 ya kifo cha Hayati Mwalimu Julius Nyerere ambaye alikua rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hafla hiyo imehudhuriwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Chama Cha  Mapinduzi (CCM) Mhe. Philip Mangula, Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi, Mkuu wa Mkoa wa Pwani  Abubakari Kunenge Ndugu Suo Peng- Naibu Balozi Mdogo na Mwakilishi wa Kikomunisti
 Chama cha China na viongozi wengine wengi ikiwamo Mabalozi wa nchi kutoka vyama rafiki.

 Luteni Jenerali Ansellm Sanyatwe - Kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Zimbabwe, wawakilishi kutoka vyama sita ambavyo ni  African 
Mwalimu Nyerere alikuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzana amefariki Oktoba  14, 1999 baada ya kuongoza nchi kwa miaka 24.
Naye Katibu Mstaafu  wa  NEC Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kanali Rungemela Lubinga amesema elimu ya historia ya harakati za Ukombozi wa Afrika na harakati za kupigania uhuru wa nchi yetu inahitajika kutolewa kuanzia Elimu ya Msingi, Sekondari na ngazi ya Vyuo Vikuu.Hayati Mwalimu Julius Nyerere amefariki Oktoba 14,1999.

Post a Comment

0 Comments