KIUATILIFU CHA KUANGAMIZA WADUDU DHURIFU THURISAVE-24CHAZINDULIWA BIOTECH

Waziri Wa Wizara ya Kilimo Hussein Bashe amezindua  kiuatilifu  hai  cha kuangamiza  wadudu dhurifu kwenye mazao kilichotambulika kama  Thurisave-24

Uzinduzi  huo umefanyika kwenye  Kiwanda Cha Viuatilifu hai Cha Tanzania Biotech Products Limited (TBPL) kilicho chini ya Shirika la  Taifa la Maendeleo  NDC kilichopo Wilayani  Kibaha, Mkoa wa Pwani.

Mhe. Bashe ametoa pongezi kwa  Kiwanda hicho kwa kutengeneza viuatilifu rafiki kwa mazingira ambavyo vinaweza kuua wadudu  ambao wamekuwa tishio katika sekta ya kilimo nchini.

Aidha Waziri Bashe  amesisitiza umuhimu wa kutumia viuatilifu hivyo na kumuelekeza Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao kuhakikisha fedha zinazotengwa kwa ajili ya viuatilifu zinatumika kununua bidhaa za TBPL na kuwafundisha wakulima jinsi ya kuvitumia ipasavyo. 
Thurisave -24 inatumika kwenye mazao ya mahindi,pamba, tumbaku,viazi vitamu ,viazi mviringo, mihogo,kabeji,mbogamboga za majani, matunda na maharagwe.
Thutisave-24  ni kiuatilifu  kisicho na madhara kinachoangamiza wadudu  waharibifu wa mazao katika hatua ya viwavijeshi kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika  bidhaa hii ina ufanisi wa hali ya juu katika udhibiti wa viwavi  wa jamii  ya  Lepidoptera.
 "Thurisave  inahakikisha  usalama wa ikolojia  na  afya za watumiaji kwakua haina sumu dhurifu na  mazingira  hivyo kutimiza malengo ya milenia"amesema Bashe.

Hafla hiyo imehudhuriwa  na Balozi wa Cuba nchini Mhe.Yordenis  Vera, Meneja TPBL  Mhandisi Rafael Moya ,Mwakilishi  wa Bodi ya NDC  Mhandisi  ,
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge wafanyakazi wa NDC.

Post a Comment

0 Comments