NYUKI WA TABORA VS FOUNTAIN GATE HAPATOSHI DIMBA LA ALI HASSAN MWINYI

Mchezaji Hussein Massalanga akizungumza  na Waandishi wa Habari hawapo pichani.

Imetolewa leo Septemba 19
Na Christina Mwagala
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Tabora United FC.

Kikosi cha Timu ya Tabora United kesho 20,Septemba  2024 kitashuka katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora  kwa ajili ya mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania bara dhidi ya Fountain Gate utakaochezwa saa kumi jioni.

Kocha Mkuu Francis Kimanzi amesema kama kuwa timu imefanya maandalizi ya kutosha kuelekea kwenye mchezo huo ambao kimsingi utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na kwamba kila mmoja anahitaji alama tatu muhimu.

Ameongeza kuwa wachezaji wa Tabora United baada ya kumaliza mapumziko wamerejea kambini wakiwa na nguvu tofauti na mchezo uliopita kwani kulikuwa na michezo mfululizo hivyo kupelekea kuwa na changamoto ya uchovu na kwamba maandalizi yamekuwa mazuri kwakuwa wamepata muda wa kupumzika.

Kwaupande wake Hussein Masalanga akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake  amesema kuwa, licha ya kufanya vizuri kwenye michezo miwili ya nyumbani, lakini changamoto kubwa iliyokuwa ikiwakabili ni ugeni wa mazingira jambo ambalo kwa sasa tayari kila mmoja ameshazoea.

Ameongeza kuwa kama wachezaji wanaendelea kuhamasishana kwenye Uwanja wa mazoezi pamoja na kambini wanapokutana ili kuhakikisha kwamba kila mmoja anatimiza majukumu yake ambayo kocha anampa na kwa asilimia kubwa kila utekelezaji umekuwa kwa umuhimu unaohitajika.

“ Ukiangalia wachezaji wengi tuliopo hapa hatukuwa msimu uliopita, bado tulikuwa tunazoea mazingira, lakini malengo yetu ilikuwa ni kupata alama sita kwenye michezo miwili tuliyocheza nyumbani mfululizo, ila sikuzote timu bora huwa haitoi sare mara mbili , hivyo tunawaahidi mashabiki zetu tutakwenda kuwapa furaha kesho uwanjani, muhimu waje kwa wingi kutuunga mkono.

Tabora United inaingia kwenye mchezo huo dhidi ya Fountain Gate ikiwa inalingana   huku ikitofautiana kwenye magoli ya kufungwa na kufunga na kwamba ipo kwenye nafasi ya nne ya msimamo na tayari imeshacheza jumla ya michezo minne ambapo kati ya hiyo imeshinda michezo miwili na kutoa sare mchezo mmoja na kupoteza mmoja.
Kocha Mkuu  wa Tabora FC Francis Kimanzi akifafanua  jambo 

Post a Comment

0 Comments