Wasanii wakitoa burudani kwenye tamasha hilo la kiutamaduni kwenye Uwanja wa Mwehe Kizimkazi Kusini Unguja .
Shamrashamra za kilele cha tamasha la Kizimkazi zikiendelea.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika kilele cha tamasha la Kizimkazi Uwanja wa Mwehe Kusini Unguja.
Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Isdor Mpango anayefuata ni msanii Hamonise,Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi wakifurahia jambo katika kilele cha tamasha la Kizimkazi kwenye Uwanja wa Mwehe Kusini Unguja.
Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ahutubia Wananchi wakati wa Kilele cha Tamasha la Kizimkazi lililofanyika katika Uwanja wa Mwehe, Kusini Unguja Zanzibar.
Rais Dkt.Samia amesema kuwa kutokana na tamasha hilo kuwa namvuto zaidi kutajengwa Uwanja wa kisasa na utakaotumika katika michuano ya Afcon utakaokuwa na uwezo kuchukua watu 20,000 na uwanja huo unatarajiwa kuwa na viwango vya kimataifa utakuwa na uwanja wa mpira wa miguu, netball, basketball na viwanja vya michezo mbalimbali ikiwemo kuogelea pia kutakuwa na sehemu ya mapumziko na uwanja wa michezo ya watoto ili kuwajengea watoto afya ya akili unatarajiwa kukamilika mapema mwakani na ujenzi wake umetoka kwa CRDB Foundation na wapenda michezo.
0 Comments