Kaimu Mkurugenzi Fedha na Utawala Chuo Cha Diplomasia Jacob Nduye akikabidhi cheti kwa mmoja ya mwanafunzi kwenye mahafali hayo.
Baadhi ya Wahitimu wa darasa la saba kutoka Shule ya Msingi Filbert Bayi yenye mchepuo wa Kiingereza za Kimara na Mkuza.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo Kaimu Mkurugenzi Fedha na Utawala Chuo Cha Diplomasia Jacob Nduye akimkabidhi cheti mwanafunzi wa kidato cha nne kwenye mahafali ya Shule ya Filbert Bayi.
MEJA Mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ambaye pia alikua mwanariadha aliyeng'ara katika medani ya mchezo wa riadha Olympic mwaka 1974 Filbert Bayi pichani juu amesema kuwa Shule yake inakabiliwa na changamoto ya miundombinu ya barabara.
Tangu nianzishe Shule hii ya Filbert Bayi changamoto kubwa tunayo kumbana nayo ni barabara kupitika kwa taabu.
"Inafika wakati natamani kusema kama tatizo ni hili jina langu ndiyo linasababisha hii barabara kutotengenezwa basi waliondoe huenda kuna watu linawakwaza lakini wakumbuke hii siyo njia yangu binafsi huku kuna wanafunzi ambao wanapitiwa kutoka Shule tofauti ,wanajeshi na wananchi wa kawaida wote wanatumia njii hii" amesema Bayi.
Meja Mstaafu Bayi amesema hayo Agosti 24 katika mahafali ya darasa la saba ya Shule ya Msingi Filbert Bayi iliyopo Kimara na Shule ya Msingi na wanafunzi wa Kidato cha nne wanaosoma Shule ya Filbert Bayi iliyopo Mkuza Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
"Nimesha fanya jitihada binafsi miaka yote tangu Shule hii ilipoanza 2006 hadi sasa ikiwa ni pamoja na kuweka mawe kwenye barabara kuchonga kwa kupitisha greda lakini sasa hivi nimechoka sababu hii siyo njia yangu binafsi" amesema Bayi.
Bayi ameongeza kwa kusema kuwa mbona zipo barabara nyingi za watu mashuhuri nyingi zinafanyiwa matengenezo kwanini hii yenye jina la Filbert Bayi haithaminiwi?amehoji Mwanariadha aliyevunja rekodi ya Olympic na Meja Mstaafu wa JWTZ.
Bayi ameongeza kwa kusema kuwa Kamati ya Bunge ambao walitembelea Shuleni hapo hivi karibuni walikwama kwenye barabara hiyo na wakampigia simu Meneja TARURA, anashukuru wananchi wamepaza sauti zao TARURA wamemwaga kifusi na kusisitiza wajitahidi kufanya matengenezo katika barabara hivyo kwani utabiri wa hali ya hewa wametoa tahadhari kuna mvua zitanyesha hivi karibuni.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo Kaimu Mkurugenzi Fedha na Utawala Chuo Cha Diplomasia Jacob Nduye amewaasa wanafunzi waliohitimu kuishi kwa kumtanguliza Mungu, kuwa na heshima na utii na kuzidisha juhudi ya msingi bora waliopatiwa shuleni hapo sambamba na kuendeleza sofa njema ya Shule hiyo kwani kuna rekodi ya wanafunzi waliohitimu shuleni hapo wengi wamepata nafasi nzuri katika ngazi za serikali na sekta mbalimbali.
Bayi anashikilia rekodi ya kukimbia KM1500 katika michezo ya Jumuia ya Madola ya mwaka 1974 aliposhinda Medali ya dhahabu.
Aidha Filbert Bayi ni Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki ya Tanzania (TOC) na hivi karibuni Agosti 6 mwaka huu amepewa heshima ya kuwa miongoni mwa wanariadha nyota waliovunja rekodi za dunia. ambapo Rais wa Shirikisho la Riadha Duniani Lord Sebastian Coe ndiyo aliandaa hafla hiyo na Bayi amejumuishwa rasmi kwenye jumba la Makumbusho la wanariadha nguli Duniani iliyopo Jijini Paris nchini Ufaransa.
Mgeni rasmi kwenye Mahafali hayo Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Chuo Cha Diplomasia Jacob Nduye kilichopo Kurasini Jijini Dar es Salaam akizungumza na wahitimu hao pamoja na wazazi kwenye mahafali hayo.
0 Comments