RAIS DK SAMIA APONGEZWA UZINDUZI WA RELI YA MWENDOKASI (SGR)





RAIS Dk Samia Suluhu Hassan amepongezwa kwa kuzindua treni ya mwendokasi ya (SGR) kwenda Dodoma kuwa ni tukio la kishujaa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa nchini.

Hayo yamesemwa Mjini Kibaha na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge wakati wa kuadhimisha Kumbukumbu ya Mashujaa kimkoa alipokuwa akizungumza na viongozi mbalimbali wa Mkoa huo.

Kunenge amesema kuwa uzinduzi huo ni jambo kubwa ambalo limeweka historia kubwa ya nchini ambapo baadhi wapinga uchumi walijaribu kuhujumu miradi mikubwa ya kitaifa lakini walishindwa.

"Wakati tukiendelea kuwakumbuka na kuwaombea mashujaa wetu tumwombee Rais kwani uzinduzi wa safari hiyo ni tukio la kishujaa na miradi mingine mikubwa ukiwemo ule wa uzalishaji umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere,"amesema Kunenge.

Amesema kuwaenzi mashujaa ambao baadhi yao wamefariki dunia na wengine wakiwa hai walifanya jambo la kishujaa la kuipigania nchi na sasa tunaishi kwa amani na upendo.

"Tuendelee kuiombea nchi yetu na Rais na viongozi wengine ili tuendelee kuienzi amani na upendo uliopo nchini udumu na tusiwape nafasi wale wanaotaka kuivuruga amani yetu iliyopo,"amesema Kunenge.

Aidha amesema anampongeza Rais kwa kuitendea haki nchi kwani atazindua mnara mkubwa wa Kumbukumbu ya Mashujaa Mnara mrefu huko Dodoma na Afrika utakuwa ni wanne.

Kwa upande wake Mchungaji Julius Shemkai amesema kuwa mashujaa hao lazima wapongezwe kwani walipambania nchi na wale wote wenye nia mbaya wasindwe ili nchi iendelee kuwa na amani.

Shemkai amesema kuwa wao viongozi wa dini wanakemea tabia iliyozuka ya kuiba watoto kwani hiyo roho haina nafasi hapa nchini.

Sheikh Said Chega alisema kuwa wanamwombea Rais ili aweze kuongoza kwa amani na kutekeleza vyema majukumu yake na nchi iendelee kubaki salama.

Chega amesema kuwa wanawaombea wale wote walioipambania nchi hadi hapa ilipofikia ikiwa na amani.

Post a Comment

0 Comments