Wanafunzi hao wakiwa katika picha na mwalimu wao wa somo la Sayansi Rashid Hamis Stambuli |
Muuguzi wa zamu kitengo cha kusafisha figo Joyce Mfyuji akiwaelekeza jambo wanafunzi hao |
Dkt bingwa wa watoto wadogo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Pius Muzzazi |
Wanafunzi hao wakiwa katika picha ya pamoja na muuguzi wa wodi ya watoto
WANAFUNZI
wa Shule ya Msingi Mchepuo wa Kiingereza ya Chalinze Modern Islamic
wamefanya ziara ya masomo kwa siku moja na kujifunza mambo
mbalimbali.
Akizungumza
kwa niaba ya wanafunzi hao Mwalimu wa Somo la Sayansi Rashid Hamisi
Stambuli amesema kuwa wanaushukuru uongozi wa Hospitali ya rufaa
Tumbi Mkoa wa Pwani kwa kuwapa fursa wanafunzi hao ambao ni Madaktari
Tarajai kwani wameweza kutimiza lengo letu kwa asilimia 99% katika
masomo ya Sayansi wanayosoma shuleni hapo.
"Hii
ni mara ya ya kwanza Shule yetu kupata nafasi ya kupata ziara ya
kimafunzo kwa vitendo wanafunzi wetu wenye ari ya kuja kuwa madaktari
wetu wa baadaye wametembelea idara tatu ambazo ni Dharura, Idara ya
kuchuja Figo na Wodi ya Watoto kuanzia umri wa siku sifuri hadi siku
28.
Akizungumza na
wanafunzi hao Daktari Bingwa wa Watoto wadogo Katika Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi Dkt. Pius Muzzazi amebainisha kuwa
miongoni mwa magonjwa yanayowaathiri watoto wadogo ni kuwa ni pamoja
na kuwa na ukosefu wa afya ya akili unaosababishwa na malezi mabovu
kutoka kwa baadhi ya wazazi ikiwa ni pamoja na kuwafokea na kuwatolea
kauli zisizofaa.
"Watoto
wengi wamekua wakipata msongo wa mawazo kutokana kupata maneno
yasiyostahili kutoka kwa watu wao wa karibu na wanao wazunguka"
amesema Dkt.Muzazzi.
Wakiwa
katika ziara hiyo Muuguzi wa zamu kitengo cha kusafisha Figo Joyce
Mfyuji amesema kuwa jamii nzima inapaswa kubadili mtindo wa ulaji kwa
sababu ndiyo chanzo kikubwa cha kuharibu figo na kusisitiza kwamba
endapo mtu ataupata ugonjwa huo itamlazimu kuchuja figo kwa kusafisha
damu mara tatu kila wiki katika muda wote wa maisha yake.
Mwanafunzi
Mussa Swedi amezungumza kwa niaba ya wenzake waliopata fursa katika
ziara hiyo ya kimafunzo amesema kuwa amejifunza kuwa siyo kila mgonjwa
huwa anapelekwa moja kwa moja kwenye wodi za watu maalumu
(ICU),"nimejifunza kwamba mgonjwa wa dharura anapofika hupokelewa na
kupewa huduma pia nimejifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamojana
kutambua kuwa kiungo kinachoitwa figo ni muhimu sanakatika maisha ya
binadamu hivyo watu wote tunapaswa kukilinda kwa kuzingatia kula mko
kamili, kufanya mazoezi.
"Pia
nimefurahi kuonanamnamgonjwa akipatiwa huduma ya kusafisha damu hili
limetujenga zaidi na kuona kaI ya Utabibu inahitaji uwe na moyo wa
kujito zaidi"amesema Mussa.
0 Comments