Fwd: JUKWAA LA WANAWAKE TANESCO LACHANGIA DAMU HOSPITALI YA TUMBI KIBAHA


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kupitia jukwaa la wanawake wa shirika hilo kwa umoja wao wamekusanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani , Tumbi Kibaha na kujitolea damu kwa ajili ya Wanawake wanaojifungua na majeruhi kadhaa wanaotibiwa katika Hospitali hiyo.

akizungumza na Waandishi wa Habari, Meneja wa Tanesco Kanda ya Pwani, Martin Maduhu amesema wafanyakazi wa shirika hilo wameamua kujitolea kwa moyo wao mara baada ya kundi la umoja wa Wanawake kufikiria kutoa mchango huo kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani.

"Sisi tumekuwa tukiwaangazia wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla kuwakikisha kuwa wanapata umeme wa uhakika lakini tumegundua umeme bila afya auna faida hivyo kupitia jukwaa hili tumeweza kuja kujitolea damua hili iweze kuwasaidia Mama zetua mabo ujifungua hapa na kumaliza damu nyingi pamoja na majeruhi."amesema Maduhu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake Tanesco , Rukia Wandwi amesema wazo hilo limekuja mara baada ya kushauriana na wenzao wa pwani na kuona umuhimu wa damu katika Hospitali iyo ambayo upokea watu wengi kuliko kawaida kutokana na barabara ya Morogoro kuwa na mikasa mingi ya ajali.

amesema kuw ahuo ni mwanzo tu kwa jukwaa hilo lakini wamejipanga kutoa msaada zaidi katika jamii hili kuaakikisha kuwa wao kama watanzania wanaona kila mmoja anakua kiuchumi na afya.

Nae Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi Kibaha,Dkt Briceson Kiwelu, aliwashukuru wafanyakazi hao wa Tanesco na kusema kuwa ni mara chache sana kuona kundi kubwa kama hilo linakuja kujitolea damu katika hospitali hiyo hivyo uwe uwe mwanzo na isiwe mwisho.

amesema kuwa uzuri wa damu inayotolewa na kundi kubwa la watu kutoka katika shirika hilo asilimia 70 huwa ni nzima kutokana na watu wake wengii huwa wanafika wakiwa tayari wamejitathmini na kuchangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa damu safi kwa muda mfupi.
  Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake Tanesco , Rukia Wandwi akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kukamilika kwa zoezi la uchangiaji Damu kwa Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanesco lilipoamua kujitolea kutoa Damu kwa jili ya Hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha mkoa wa pwani kama Sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
 Meneja wa Tanesco Kanda ya Pwani, Martin Maduhu akizungumza jinsi gani Tanesco inavyoweza kuwaangazia wananchi maisha yao kwa kushiriki katika utoaji damu kwa ajili ya kuwezesha wajawazito na watu wanaopata ajali waweze kupata matibabu haraka katika Hospitali ya Tumbi Kibaha mkoani Pwani.
 Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi Kibaha,Dkt Briceson Kiwelu akitoa neno la ukaribisho kwa wafanyakazi wa Tanesco wa Dar es Salaam na Pwani waliojitokeza kwa wingi kujitolea Damu kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yatakayo adhimishwa Marchi  8  mwaka huu
 Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake Tanesco , Rukia Wandwi akiwa katika Maandalizi ya utoaji wa Damu katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Pwani Tumbi Kibaha.
Mmoja ya Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanesco ambaye ni Mwanachama wa Jukwaa la Wanawake wa Shirika hilo akiwa katika vipimo vya awali kwa ajili ya uchangiaji damu katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Pwani tumbi Kibaha.
 Mmoja ya Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanesco akiendelea na zoezi la utojai Damu kwa ajili ya Wagonjwa watakaofika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani ,Tumbi Kibaha
 Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake Tanesco , Rukia Wandwi, akichukuliwa vipimo vya mapigo ya moyo kabla ajaingia katika zoezi la utoaji damu
 Sehemu ya Wafanyakazi wa Tanesco na wanachma wa jukwaa la Wanawake wa Shirika hilo wakiwa katika foleni ya kusubiri kuingia kwenda kuchangia Damu katika Hospitali ya Tumbi Kibaha
  Sehemu ya Wafanyakazi wa Tanesco na wanachma wa jukwaa la Wanawake wa Shirika hilo wakiwa katika foleni ya kusubiri kuingia kwenda kuchangia Damu katika Hospitali ya Tumbi Kibaha
Baadhi ya wana jukwaa wakiimba kuhamasishana uchangiaji damu kwa hiyari.

Post a Comment

0 Comments