Rais mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete akifurahi kuona papai alililopelekewa na Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita/Livinggreen) walipokwenda kumpa elimu kuhusu kilimo bora cha zao hilo nyumbani kwake Msoga, Chalinze mkoani Pwani. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange.
Dk. Kikwete akishukuru kwa mafunzo hayo yaliyotolewa na Mwanachama wa Mkikita Mtaalamu wa Kilimo cha Papai kutoka Kampuni ya Awino Farm, Ezra Machogu. Kulia ni Adam NGAMANGE
Na Richard Mwaikenda, Msoga,
.RAIS mstaafu Dk.Jakaya Kikwete amefurahishwa na elimu ya kilimo cha kisasa cha Papai chenye
gharama nafuu aliyopatiwa na Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita/Living green)
Elimu hiyo ilitolewa hivi karibuni nyumbani kwake Msoga, Chalinze, mkoani Pwani na Ezra Machogu Mtaalamu wa Kilimo wa Kampuni ya Awino Farm ambayo ni mwanachama wa Mkikita.
Kikwete alifurahi kuambiwa kwamba kampuni hiyo inaweza kuzalisha papai lenye ubora kwa
kutumia teknolojia ya kisasa yenye gharama nafuu hivyo kumfanya mkulima apate faida kubwa
wakati wa mauzo.
Ezra anasema kuwa unaweza kupunguza gharama kwa kuacha kuchimba mashimo badala yake
unalima shamba mara tatu kwa kutumia trekta, hivyo kuufanya udongo kuwa tifutifu kitendo
kitakacho kurahisishia kupanda miche ya papai bila matatizo.
Anasema ukitumia njia hiyo itakuondolea gharama ya kuchimba mashimo 1200 katika heka
moja ambayo jumla ni sh. mil. 6 ikiwa kila shimo itakuwa sh. 500 wakati kulima mara tatu
heka moja kwa trekta ni sh. 150,000.
Ezra anamweleza Dk. Kikwete kuwa unaweza pia kupunguza gharama ya mbolea kwa kila shimo
kuweka majagi mawili badala ya debe moja.
Pia alimweleza kuwa katika umwagiliaji papai halihitaji maji mengi, hivyo unaweza kutumia
lita 10,000 kwa siku kumi badala ya siku nne.
Alisema kuwa pia wamejipanga kimasoko kwa kuutumia mtandao wa Mkikita ambao tayari una
watalaam wa masoko ya ndani na nje ya nchi pamoja na watalaamu wa kufungasha (Packaging)
bidhaa kwa teknolojia ya kisasa.
Baada ya kuridhika na maelezo hayo, Rais mstaafu, alifurahi na kuishukuru Mkikita kwa
kumpelekea watalaam hao kutoka Kampuni ya Awino Farm.
Ezra alizidi kumfurahisha, Dk. Kikwete kuwa kwa heka moja akiuza papai anaweza kupata hadi
sh. mil. 80,000,000 kwa mchanganuo ufuatao;
Heka moja inaweza kupandwa mipapai 1000 hadi 1200 na kwamba mpapai mmoja unaweza kuzaa
papai 100 hadi 1300 na endapo kila papai lenye uzito wa kilo 2 likiuzwa kwa bei ya jumla sh.
800 ukizidisha na wastani wa papai 100 kila mche halafu zidisha kwa miche 1000 tu unapata
kiasi hicho cha fedha kwa msimu wa kwanza.
Pia alimueleza kuwa uzuri wa miche ya papai huishi miaka mitatu ambapo kila wiki utakuwa
unavuna na kuuza, hivyo kukupatia faida kubwa tofauti na mazao mengine ambayo ukivuna mara
moja tu.
"Laiti kama ungekuwa mchungaji, padri au sheikh anayehubiri kutafuta waumini, basi bila
shaka mimi mmenipata nimekuwa muumini wenu." Alisema Dk. Kikwete huku akicheka kwa furaha.
"Kubwa mlilonifurahisha ni jinsi mlivyopunguza kwa kiasi kikubwa gharama ya kuzalisha papai
na faida kubwa nitakayoipata, nipo tayari kutoa heka 10 za kuanzia."Aliahidi Dk. Kikwete
ambaye alisema kazi ya kilimo anaipenda na kwamba iko kwenye damu yake.
Ujumbe huo uliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita Adam Ngamange, ambaye akabla y yote alimshukuru Dk. Kikwete kwa kuwaalika na kumuomba ajiunge na mtandao, jambo ambalo
alilikubali.
Ujumbe alioongozana nao ni Ezra Machogu, Martine Wamaya wa Kampuni ya Awino Farm,
Khalid Tamim, Hassan Tamim na Ali Said ambao ni Wawekezaji wa zao la muhogo, Mkurugenzi
Betl Worldwide Ltd, Murtaza Bharmal ambaye ni mtaalamu wa masoko na uongezaji thamani mazao na Richard Mwaikenda ambaye ni Mshauri wa Habari wa mtandao huo.
Meneja Kilimo wa Mashamba ya Dk. Kikwete, Justine (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Awino, Martine Wamaya (kulia) na Mtalaamu wa kilimo cha Papai, Ezra Machogu walipokuwa wakitoka kuchuma papai kutoka kwenye shamba darasa la Kampuni ya Awino eneo la Msata tayari kumpelekea Rais mstaafu, Dk. Kikwete. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Dk. Kikwete akisalimiana na Adam Ngamange wa Mkikita
Dk. Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Awino Farm, Wamaya.
Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mtaalamu wa Kilimo cha Papai, Ezra
Dk. Kikwete akisalimiana na wanachama wa Mkikita wawekezaji katika shamba la Muhogo. Kushoto ni Khalid Tamim na Hassan Tamim.
Meneja wa Kilimo wa Mashamba ya Dk. Kikiwete, Justine akiutambulisha ujumbe wa Mkikita nyumbani kwa Kikwete, Msoga
Ngamange akielezea mbele ya Dk Kikwete kuhusu utendaji wa mtandao huo
Mtaalamu wa Kilimo cha Papai, Ezra (kulia) akitoa elimu kwa Dk. Kikwete kuhusu kilimo bora cha zao hilo kwa gharama nafuu
Ngamange akimkabihi Dk. Kikwete mafuta yaliyotengenezwa kwa kutumia mchaichai
Dk. Kikwete akifungua kasha la mchaichai
Mtaalamu wa Masoko na Ufungashaji wa bidhaa mshirika wa Mkikita, Murtaza Bharmal (kulia) akitoa maelezo jinsi anavyoweza kutafuta masoko kirahisi kwa kutengeneza makasha mazuri ya kuhifadhia bidhaa ili kuongeza thamani.
JK akiwa na ujumbe wa Mkikita pamoja maofisa wasaidizi wake
Dk. Kikiwete akizungumza Ngamange (kulia) pamona na Murtaza
JK akiagana na kiongozi wa ujumbe wa Mkikita, Ngamange baada ya ziara yao kumalizika
JK akiagana na mwandishi wa habari wa Azam TV, Octor

Dk. JK akinusa mafuta hayo ya mchaichai |

0 Comments