Katika siku za hivi karibuni, kumejitokeza tabia kwa baadhi ya watu wakiwemowasanii watu
wengine mmoja mmoja kutumia mavazi yanayofanana na sare za Majeshi ya Ulinzi na
usalama hapa nchini likiwemo Jeshi la Polisi katika shughuli zao za kisanii au
katika kazi mbalimbali, Jambo ambalo ni kinyume cha sheria,kanuni na taratibu
za Nchi.
Kwa mujibu wa Sheria ya kanuni za makosa ya Jinai, sura ya
16 na marejeo yake ya mwaka 2002, kifungu cha 178 (1) na (2)
kinachozungumzia makosa dhidi ya sare za
majeshi ya ulinzi na usalama,
kinabainisha wazi kuwa ni kosa
kisheria kwa mtu yeyote ambaye siyo mtumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama
kuvaa mavazi yanayotumiwa au kushabihiana na sare za majeshi hayo bila kibali kutoka kwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kufuatia kitendo
kilichofanywa na kundi la kisanii la “ Original Comedy” kuvaa mavazi
yanayoshabihiana na sare za Jeshi la Polisi,Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya
Dar Es Salaam linachukua hatua za
kisheria dhidi ya wasanii hao.
Aidha Jeshi la Polisi nchini, linatoa onyo kali kwa mtu ama
kikundi chochote kuacha kutumia mavazi
yanayofanana na sare zinazovaliwa na majeshi ya ulinzi na usalama hapa nchini na atakayebainika hatutasita kuchukua hatua
kali za kisheria dhidi yake.
Jeshi la Polisi linatoa
rai kwa wale wote wenye mavazi yanayoshabihiana na sare za majeshi ya
ulinzi na usalama
kuzisalimisha mara moja katika
vituo vya Polisi vilivyokaribu nao.
Imetolewa na:
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Advera John Bulimba –
Kamishna
Msaidizi wa Polisi (ACP)
0 Comments