MSIMU MPYA UNAKUJA WA SUPER SPORT



NA MWANDISHI WETU

Ulimwengu wa Mabingwa Super Sport katika kuwajali mashabiki wake umepanga kuwaletea soka bora barani Afrika kwa kuonyesha michuano yote moja kwa moja ya msimu mpya katika kiwango cha HD kupitia DStv.

Hayo yalisemwa jana na Ofisa Msoko wa DStv Furaha Samalu katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika ofisni kwao Jijini Dar es Salaam.

“Mashabiki wa soka mlipatiwa kionjo cha msimu ujao wa soka mwishoni mwa wiki iliyopita wakati DStv ilipoonyesha pambano lililokuwa linasubiriwa kwa hamu la kugombea Ngao ya Hisani ambalo lilishuhudia Man United wakitwaa kombe la kwanza mbele ya mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza msimu uliopita, Leicester City” .

Alisema mechi zote 380 zitaoneshwa kupitia DStv. Alisema kwa uhakika nchi zisizopungua 300 zitaonyeshwa moja kwa moja kitu ambacho kinathibitisha kwamba Supersport ndiyo mpango mzima kwa wapenzi na watazamaji wa soka na matukio mengine ya kimichezo barani Afrika.

Chaneli hii ya michezo hukuletea matangazo kwa mapana na marefu ambayo hujumuisha uchambuzi wa kina wa Premier League kutoka kwa wachambuzi mahiri wa soka ambao hawana upinzani kokote barani Afrika.

Aliongeza kwa kusema kuwa msimu hii unaokuwja utaleta kivutio kikubwa zaidi kuku Premier League ikiwa na mechi za siku ya Ijumaa kwa mara ya kwanza.
Mechi hizo zitaanza saa kumi jioni kwa saa za Afrika ya Kati ambapo Super Sport itakuwa inarusha mechi tatu za ziada kwa wakati mmoja kupitia chaneli mbalimbali za Super Sport SS3, SS5,SS6,SS7,na SS11 huku Chaneli maarufu ya Premier League itaendelea kuwepo kupitia SS11 kuendelea kuthibitisha kwamba Super Sport ndiyo makazi ya soka la kimataifa.

Post a Comment

0 Comments