Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Kulia) akiwaeleza jambo
viongozi wa CUF walioongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Mhe. Maalim
Seif Sharif Hamad (Katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Julius Mtatiro
waliomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo Agosti 13, 2016. Mhe.
Spika, Job Ndugai amerejea nchini hivi karibuni akitokea nchini India
alikokwenda kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.
Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Kulia) akifurahia jambo na
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad
(Katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Julius Mtatiro waliomtembelea
nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo leo Agosti 13, 2016 .
Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Kulia) akimweleza jambo Katibu
Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto)
aliyeambatana na viongozi wenzake wa CUF nyumbani kwa Mhe. Spika Job Ndugai
leo leo Agosti 13, 2016 jijini Dar es salaam.
Naibu katibu mkuu wa
CUF, Bara na Mbunge wa Kaliua, Tabora Mhe. Magdalena Sakaya akimweleza
jambo Mhe. Spika, Job Ndugai (hayupo pichani) mara baada ya kumtembelea Mhe.
Spika leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF
Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad.
Viongozi wa Chama cha
Wananchi CUF wakimwombea dua Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Job Ndugai (kulia) ili aendelee kuwa na afya njema ya kumuwezesha
kutekeleza majukumu yake kikamilifu walipomtembelea nyumbani kwake leo jijini
Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Chama
Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (Kushoto) akimuaga Spika wa
Bunge Mhe. Job Ndugai mara baada ya kumtembelea nyumbani kwake leo jijini Dar
es salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa
Chama cha Wananchi CUF, Julius Mtatiro akimuaga Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai
mara baada ya kumtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam. Viongozi wa CUF
wamefika nyumbani kwa Mhe. Spika, Job Ndugai kumjulia hali baada ya kurejea
hivi karibuni akitokea nchini India alikokwenda kwa ajili ya uchunguzi na
matibabu. Picha/Aron Msigwa
–MAELEZO.
0 Comments