KOCHA MKUU WA TAIFA STARS CHARLES MKWASA AITA NYOTA 20 WAKUIVAA NIGERIA

Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa, ametangaza wachezaji 20 watakaounda kikosi kitakachosafiri mwishoni mwa mwezi huu kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, Super Eagles. Licha ya mchezo huo wa Septemba 3, 2016 kuwa sehemu ya mchuano wa kuwania nafasi ya kucheza fainali hizo za AFCON 2017 huko Gabon, lakini utakuwa ni wa kukamilisha ratiba baada ya Misri kufuzu kutoka kundi G ambalo mbali ya Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo iliyojitoa katikati ya mashindano. “Tanzania hatuwezi kupuumza mchezo huu, tumeuchukulia serious (kwa umakini) kabisa kwa sababu tunacheza ugenini ambako matokeo mazuri yanaweza kutusongesha mbele na kuingia ndani ya timu 99 bora katika viwango vya FIFA,” amesema Mkwasa. Katika kikosi chake, Mkwasa ametangaza kutomjumuisha Mshambuliaji wa Kimataifa, Thomas Ulimwengu anayecheza klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kutokana na majeruhi ya paja kama ilivyo kwa Juma Abdul wa Young Africans ambaye aliumia katika mchezo wa kuwania Kombe la Shirikisho dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria. “Timu itaingia kambini Agosti 28, itakaa kambini kwa siku tano kabla ya kusafiri kucheza mchezo huo wa kukamilisha ratiba ambao Misri tayari wameshafuzu fainali za Afrika,” amesema Mkwasa na kuongeza kuwa kuna mchezaji wa Tanzania, Said Carte Mhando anamfuatilia ili ikiwezekana baadaye amwite kuchezea timu ya taifa. Anakipiga Klabu ya Brencia Calcio ya Italia. Wachezaji walioitwa: Makipa Majina ya timu zao kwenye mabano Deogratius Munishi (Young Africans), Aishi Manula (Azam FC), Mabeki Kelvin Yondani, Vicent Andrew, Mwinyi Haji (Young Africans), Mohamed Hussein (Simba SC),Shomari Kapombe na David Mwantika (Azam FC). Viungo ni Himid Mao (Azam FC),Shiza Kichuya, Jonas Mkude na Muzamiru Yasin (Simba SC),Ibrahim Jeba (Mtibwa Sugar),Juma Mahadhi (Young Africans)na Farid Mussa Tenerif ya Hispania Huku safu ya washambuliaji ni Simon Msuva (Young Africans), Jamal Mnyate, Ibrahim Ahib(Simba SC) na John Bocco (Azam FC)

Post a Comment

0 Comments