NZAGAMBA YAFANYA KWELI



Meneja mauzo na usambazaji wa Nzagamba Taifa Fred Kazindogo akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mwanza juu ya kuzinduliwa kwa ppromoshesheni ya kuwazawadia watumiaji wa Nzagamba kujishindia Ngombe kumi kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa,Kulia ni Meneja Masoko wa Nzagamba Oscar Shelukindo.


Na Mwandishi Wetu, Mwanza
PROMOSHENI ya aina yake imezinduliwa kwa watumiaji wa bia ya asili ya Nzagamba, ambapo ng’ombe dume 10 watashindaniwa.

Bia hiyo inayozalishwa Mwanza na Kiwanda cha Nzagamba kilicho chini ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imeamua kuendeleza promosheni hiyo kwa mwaka wa pili mfululizo itakayojulikana kama ‘Win A Bull’ (Shinda Ng’ombe Dume) kuanzia jana.

Akizungumza katika uzinduzi wa promosheni hiyo inayotarajiwa kuwa kivutio kikubwa kwa watumiaji wa bia ya Nzagamba na wananchi wote kwa ujumla, Meneja Masoko wa Nzagamba, Oscar Shelukindo alisema itaishia Agosti 27, mwaka huu.

“Leo (jana) tuna furaha kubwa kufanya uzinduzi wa promosheni hii ya aina yake kupitia bia yetu ya asili ya Nzagamba.  Kama lilivyo jina la bia hii Nzagamba inamaanisha ‘Ng’ombe Dume’ hivyo tumeona ni vema washindi wa promosheni hii wakajishindia zawadi ya ng’ombe huyo.

“Pamoja na zawadi hizi kubwa za ng’ombe pia tutakuwa na zawadi ndogo ndogo zitakazotoka kila wiki katika promosheni zitakazofanyika maeneo mbalimbali katika Kanda ya Ziwa,” alisema Shelukindo.

Meneja Mauzo na usambazaji wa Kampuni ya DarBrew walio wazalishaji wakuu wa kinywaji hicho, Fred Kazindogo alisema, ng’ombe hao watatolewa sehemu mbalimbali za Kanda ya Ziwa.

Alizitaja kanda walizozigawanya kuwa ni Ilemela, Nyamagana, Sengerema, Geita, Kakola, Kahama, Maswa, Bariadi, Magu na Majita.

Mratibu wa shindano hilo, Peter Mwambenja alisema, ili kushiriki promosheni hii na kushinda zawadi, mteja wa Nzagamba anatakiwa anunue bia mbili katika baa au sehemu atakapokuwa anapata kinywaji, kisha atapatiwa fomu maalumu atakayojaza jina lake, mahali alipo na mawasiliano yake.

“Mwisho wa promosheni zitafanyika droo kubwa ambapo washindi watakabidhiwa zawadi zao za n’gombe dume yaani ‘Nzagamba’ na kuondoka nayo. 

“Tunawasihi wateja wa bia hii ya Nzagamba kushiriki kwa wingi ili wajishindie zawadi hizi maalumu kwa ajili yao,” alisema Mwambenja.

Shelukindo alisisitiza wateja kuiamini Nzagamba na kuitumia kwani ni moja kati ya kinywaji kinachomsaidia mtu kujenga afya yake.

“Nzagamba ni moja kati ya bia bora zaidi, kwani mbali na yote pia inatengenezwa kwa kutumia mazao ya hapa nchini, huku ikiandaliwa katika mazingira bora zaidi,” alisema.

Bia ya asili ya Nzagamba inazalishwa zaidi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kupitia TBL moja kati ya kampuni kubwa na zenye mafanikio ya aina yake hapa nchini.

Post a Comment

0 Comments