ZOEZI LA UKOAJI GARI TOYOTA HIACE NA MIILI MIWILI LAKAMILIKA



Zoezi la uokoaji Gari aina ya Toyota Hiace lililozama baharini leo tarehe 20/04/2015 saa 10 alfajiri, likiwa na watu wawili, limekamilika saa 12:00 jioni hii, baada ya miili hiyo kutolewa kwenye maji na gari hilo kupatikana.

 Gari hilo lililokuwa kwenye MV. Kigamboni kutokea upande wa Magogoni kuelekea upande Kigamboni, likiwa imeegeshwa ndani ya kivuko, ghafla lilitoka kwenye kivuko na kuzama baharini likiwa na dereva mmoja na abiria mmoja.

 Shughuli za uvushaji abiria magari na mizigo siku ya leo zimeendelea kwa vivuko vyote viwili TEMESA inapenda kutoa wito kwa watumiaji wa vivuko vyote kuzingatia maelekezo yanayotolewa na mabaharia wanaofanya kazi kwenye vivuko hivyo.

 Uongozi wa TEMESA unatoa pole kwa ndugu na jamaa wa marehemu walio poteza maisha. Aidha uongozi wa TEMESA unatoa shukrani kwa wale wote waliofanikisha zoezi la ukoaji wakiwemo; Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, Kikosicha Jeshi la Wanamaji, Mamlaka ya Bandari, Polisi Kikosi cha Maji pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali waliofika eneo la tukio.

Imetolewa na Ofisi ya Mtendaji Mkuu TEMESA

Post a Comment

0 Comments