"Nimepokea kwa Masikitiko Makubwa Taarifa za Kifo cha Mzee wetu Mzee Mapili...
Breaking News.... Tanzia.... Mwanamuziki Mkongwe Kassim Mapili amefariki leo jioni baada ya kuonekana hajatoka Chumbani kwake kwa Muda Mrefu.... Ndipo mlango ukavunjwa nyumbani kwake Tabata Matumbi."alisema November.
Mzee atakumbukwa kwa Kibao cha Napenda Nipate Lau Nafasi na Rangi Ya Chungwa....
Taarifa zaidi zitawajia...!! Plz call 0744150000 Kama una swali... Nawaomba wanamuziki wote Tujitoe kwa wingi kumpa heshima Mzee wetu Mapili....!! Addo November Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania..!!
Novemba alisema kuwa msiba huu ni mkubwa katika tasnia ya muziki nchini huku akiwataka wasanii wajitokeze katika msiba huo.
Alisema kuwa hivi karibuni marehemu alikua akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo na alikua akihudhuria Clinic ya moyo, "Jana aliangalia mpira akiwa na vijana wake na alipoingia kulala hakutoka tena jambo ambalo liliwashtua vijana wake kutokana na ukimya huo ndipo walipokwenda kutoa taarifa Kwa jeshi la Polisi walipokuja wakavunja mlango na kuukuta mwili ndani akiwa amesha fariki" alisema November.
ALIYEUA NA KUMZIKA MTOTO WAKE SHAMBA LA MAHINDI NA PAMBA GEITA ATIWA MBARONI
-
Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mtuhumiwa Masanja Mihayo, Miaka
31, Mkulima, Mkazi wa Ikandilo Wilaya ya Geita kwa tuhuma za mauaji ya
mtoto ...
1 hour ago
0 Comments