Mamia ya wakazi wa Dar es Salaam na Kibaha Mkoa wa Pwani wamejitokeza kwa wingi katika mazishi ya aliyekua bondia mkongwe Lucas Msomba.
Akizungumza katika Ibada ya mazishi Bondia Emmanuel Mlundwa amemuelezea marehemu Msomba kuwa alikua msukuma masumbwi mwenye uwezo na kipaji kikubwa katika ulingo wa ngumi nchini enzi za uhai wake.
Marehemu Msomba alizaliwa 1957 na amezikwa leo tarehe 12 Aprili 2026 katika makaburi ya Msangani yaliyopo Kwa Matias Wilayani Kibaha Mkoa Pwani.
"Nlicheza na Msomba katika michuano mbalimbali ikiwa ni pamoja na michuano ya Kimataifa ambapo tulikuwa katika timu ya taifa ya ngumi".
"Mwaka 1976 tulikuwa wote kwenye timu ya taifa ya ngumi ambapo tulikuwa tumepangwa kwenda kupeperusha bendera ya taifa kwenye michuano ya Olympic lakini hatukwenda baada ya Bara la Afrikakujutoa" amesema Mlundwa.
Ameongeza kwa kusema kuwa mwaka 1980 walikwenda kwenye michuano ya Olympic ambapo mimi nilitwaa medali ya fedha na Msomba akashinda medali ya Shaba" amesema Mlundwa.
Naye Bondia wa zamani Ngoya Mbise amemuelezea marehemu Msomba kuwa alikua mpiganaji katika uzito wa Light Walter Weight pia alikua mchezaji mzuri na mwenye rekodi nzuri katika masumbwi nchini.
" Nakumbuka mwaka 1979 nilizichapa naye kwenye mashindano ya Shimuta yaliyofanyika Mwanza na akanishinda kwa Pointi." amesema Mbise.
Marehemu Bondia Msomba ameacha mjane watoto watatu na wajukuu 12 .Sisi ni wa Mwenyeezi Mungu na kwake tutarejea apumzike kwa amani.


0 Comments