Mwanamuziki mkongwe nchini Kassim Mapili wa kwanza kulia katika enzi za uhai wake amefariki dunia ghafla nyumbani kwake leo.Jumatatu wiki hii marehemu alionekana kwenye mazishi ya mwanahabari Fred Mosha na alionekana mwenye afya katika mazishi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Mwaka mmoja uliopita marehemu aliwahi kusumbuliwa na maradhi ya koyo na kuvimba miguu hali iliyopelekea kulazwa katika Taasisi ya Moyo inayofahamika kwa jina la Jakaya Kikwete iliyopo ndani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Blogu hii inaungana na wadau wote wa muziki wa dansi katika msiba huu wa mzee wetu aliyekua mcheshi wakati wote na aliyekua hajiweki nyuma kwenye masuala ya muziki wa dandi huku akiupigania ikiwa ni pamojana kutoa ushirikiano wa kimtazako , mbinu na mawazo mbalimbali pale alipohitajika na wanamuziki wa rika zote.
Innalillahwainailaihwainnailaihrajiun
SERIKALI YATOA BILIONI 14.4 MRADI WA ENGARUKA
-
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika leo Januari 10,2025 katika tarafa ya
Mtowambu w...
1 hour ago
0 Comments