BUZWAGI YAWAZAWADIA WAFANYAKAZI BORA WA MWAKA



Meneja wa Idara ya Maboresho ya Biashara wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Richard Ojendo wa kwanza kushoto akipokea tuzo ya heshima ya utumishi uliotukuka ya meneja wa mgodi, “General Manager Prestegious award” kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Bwana Benson Mpesya,(katikati) anaeshuhudia upande wa kulia ni Eng. Philbert Rweyemamu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini aliyekuwa Shinyanga.

Meneja wa Idara ya Maboresho ya Biashara wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Richard Ojendo wa kwanza kushoto, mkuu wa wilaya ya Kahama bwana Benson Mpesya na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi wakiwa katika picha ya pamoja na Bwana Ojendo mara baada ya kutunukiwa uzo ya  akipokea tuzo ya heshima ya utumishi uliotukuka ya meneja wa mgodi, “General Manager Prestegious award”.
Meneja wa Idara ya Madini wa Mgodi wa Buzwagi Eng. Muganda Mutereko wa kwanza kushoto akipokea tuzo ya Meneja Bora wa Mwaka ”Best Manager of the year” kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Bwana Benson Mpesya,(katikati) anaeshuhudia upande wa kulia ni Eng. Philbert Rweyemamu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi.
Meneja wa Idara ya Ufanisi wa Kampuni wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Saimon Sanga wa kwanza kushoto akipokea tuzo ya ya mshindi wa pili kwa nafasi ya Meneja Bora wa Mwaka ”Best Manager of the year” kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Bwana Benson Mpesya,(katikati) kulia ni Eng. Philbert Rweyemamu.
Mkuu wa kitengo cha Uchenjuaji wa Dhahabu wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Festo akimpokelea Tuzo ya Mshindi wa tatu Bwana Karel Schultz ambaye ni meneja wa Kinu cha Uchenjuaji wa Mgodi wa Buzwagi mara baada ya kutangazwa mshindi wa tatu katika nafasi ya Meneja Bora wa Mwaka ”Best Manager of the year” tuzo hiyo ilikabidhiwa na mkuu wa wilaya ya Kahama Bwana Benson Mpesya.
Washindi wa Tuzo ya Meneja bora wa mwaka wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi.(kutoka kushoto ni Saimon Sanga Meneja wa Idara ya Ufanisi, wa pili ni Eng. Muganda Mutereko Meneja wa Madini, wa tatu ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Bwana Benson Mpesya na wa nne ni Eng.Philbert Rweyemamu aliesimama upande wa kulia ni bwana Festo aliyepokea tuzo hiyo kwa niaba ya bwana Karel Schultez
Mkuu wa kitengo cha Load and Haul Bwana Marco Peter wa kwanza kushoto akipokea tuzo ya Mfanyakazi bora wa mwaka ”Best employee of the year” kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Bwana Benson Mpesya,(katikati) aliyesimama upande wa kulia ni Eng. Philbert Rweyemamu.
Bwana Gulam Fazal Mkuu wa kitengo cha Ghala(warehouse) wa kwanza kushoto akipokea tuzo ya mshindi wa pili wa nafasi ya Mfanyakazi bora wa Mwaka “Best employee of the year” anaekabidhi tuzo hiyo ni mkuu wa wilaya ya Kahama Bwana Benson Mpesya,(katikati) kulia ni Eng. Philbert Rweyemamu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi.
Waziri Selemani Mkuu wa kitengo cha Huduma za Nje (Outside Services) wa kwanza kushoto akipokea ngao ya mshindi wa yatu baada ya kuibuka mshindi wa nafasi hiyo katika kundi la wafanyakazi bora wa Mwaka anaemkabidhi tuzo hiyo ni mkuu wa wilaya ya Kahama bwana Benson Mpesya ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.
Washindi wa tuzo za mfanyakazi bora wa Mwaka “Best Employee of the Year” wakiwa katika picha ya pamoja na meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Eng, Philbert Rweyemamu na Mgeni Rasmi mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Benson Mpesya.
Washindi wa tuzo za mfanyakazi bora wa Mwaka, meneja bora wa mwaka na mshindi wa tuzo ya heshima ya utumishi uliotukuka ya meneja mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Eng, Philbert Rweyemamu na Mgeni Rasmi mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Benson Mpesya.
Bwana Amos John(Kushoto) ambaye ni Meneja wa Idara ya Biashara Mgodi wa Buzwagi akimkabidhi cheti Bwana James Jisena kama sehemu ya kutambua mchango wake kwa kampuni kwa utumishi wa muda mrefu.
Bwana Amos John(Kushoto) ambaye ni Meneja wa Idara ya Biashara Mgodi wa Buzwagi akimkabidhi cheti mmoja wa wafanyakazi wa Idara yake kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi kirefu.
Meneja wa Idara ya Uendelevu  wa Mgodi wa Buzwagi Bwana George Mkanza  akimkabidhi cheti Bwana Abdalah kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi kirefu.
Meneja wa Idara ya Madini wa Mgodi wa Buzwagi Eng. Muganda Mutereko  akimkabidhi cheti Wilbert Masawe kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi kirefu
Meneja wa Idara ya Huduma za kitaalamu za madini Bwana Sam Eshun akimkabidhi cheti mmoja wa watumishi katika idara yake kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi kirefu.
Meneja wa Idara ya Madini wa Mgodi wa Buzwagi Eng. Muganda Mutereko  akimkabidhi cheti Cosmas Joseph kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi kirefu.
Meneja Mkuu wa Idara ya Ufanisi wa Kampuni ya Acacia Bi. Janet Ruben akimkabidhi mmoja wa wafanyakazi cheti  kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi kirefu katika idara ya Ufanisi wa Kampuni katika Mgodi wa Buzwagi
Meneja Mkuu wa Idara ya Ufanisi wa Kampuni ya Acacia Bi. Janet Ruben akimkabidhi Victor Mtutwa kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi kirefu katika idara ya Ufanisi wa Kampuni katika Mgodi wa Buzwagi.

Meneja Mkuu wa Idara ya Ufanisi wa Kampuni ya Acacia Bi. Janet Ruben akimkabidhi Shamsa Mohamed kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi kirefu katika idara ya Ufanisi wa Kampuni katika Mgodi wa Buzwagi
Meneja wa Idara ya Assets Reliability Eng. Peter Mbawala akikabidhi cheti Agness Joseph kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi cha miaka mitano
Mkuu wa kitengo cha Idara ya Raslimali watu Bwana Ivocatus Masanja akitangaza majina ya washindi wa Tuzo mbalimbali ambazo zilitolewa wakati wa halfa ya siku ya familia ya Mgodi wa Buzwagi.
Mshauri Mkuu wa Idara ya Uendelevu wa kampuni ya Acacia Steve Kisyaki (kushoto) akimkabidhi cheti Bwana Franco Eliya Mwakalinga kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi kirefu.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Eng.Philbert Rweyemamu akizungumza na wafanyakazi wa Mgodi wa Buzwagi pamoja na familia zao mara baada ya kuwatunuku tuzo mbalimbali na vyeti baadhi ya wafanyakazi waliofanya vizuri katika kipindi cha mwaka 2015
Kutoka kulia ni Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa Mgodi wa Buzwagi Bi Blandina Munghezi na Magesa Magesa Afisa Mawasiliano wa Mgodi wa Buzwagi (Kulia) wakifafanua jambo kwa mshereheshaji wa shughuli hiyo MC kalinga. (katikati)
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya (wa kwanza Kulia) akifurahia jambo na meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Eng.Philbert Rweyemamu (katikati) wakati wa hafla ya kutoa tuzo kwa wafanyakazi bora pamoja na kuadhimisha siku ya familia ya wafanyakazi wa Buzwagi.
BURUDANI YA KUKATA NA SHOKA NAYO HAIKUKOSEKANA VIJANA WA JJ BAND KUTOKA MWANZA WAKAUFANYA USIKU WA FAMILIA YA BUZWAGI KUWA WA AINA YAKE.

Post a Comment

0 Comments