TANAPA WAHAMASISHA WANANCHI KUTEMBELEA HIFADHI ZA TAIFA


Baadhi ya Maofisa kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa,TANAPA, pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii wakizungumza na wanahabari (hawako pichani ) juu ya kampeni ya kuhamasisha wananchi kutembelea hifadhi za taifa ambapo katika kipindi cha miezi sita watakao tembelea zaidi ya Hifadhi nne watapata ofa ya kutembelea Serengeti ikiwa ni pamoja na kugharamiwa maradhi katika hoteli yenye hadhi ya nyota tano.
Kaimu Meneja Mauzo wa TANAPA,Victor Ketansi akisisitiza jambo.
Mkuu wa Idara ya Utali katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Eva Mallya akizungumza vivutio mbalimbali vunavyopatikana katika hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro.

Mwakilishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye pia ni afisa utalii mfawidhi na mkuu wa kanda ya utalii Kaskazini,Lauriano Munishi akizungumza jambo mbele ya wanahabari
          (hawako pichani)juu ya uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha utali wa ndani.
Mkuu wa Idara ya Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha,(ANAPA) Neema Philip akizungumzia vivutio mbalimbali vinayopatikana katika hifadhi ya Arusha.
Afisa Utalii Mwandamizi katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ,Pellagy Marandu akizungumzia vivutio mbalimbali vinavyoopatikana katika hifadhi hiyo.
Meneja Mawasiliano Mwandamizi wa Shirika la Hifadhi za Taifa,TANAPA,Catherine Mbena akiwa na mwandishi wa habari wa TBC Kilimanjaro,Sauda Shimbo wakati wa kikao cha maofisa wa TANAPA na wanahabari kuzungumzia juu ya kampeni ya kuhamasisha wananchi kutembelea hifadhi za taifa .

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini

Post a Comment

0 Comments