Na Dixon
Busagaga.Moshi.
MAMLAKA ya maji
safi na usafi wa Mazingira
mjini Moshi(MUWSA) inakusudia kuongeza bei ya kutoa huduma za maji kwa
watumiaji wake ,lengo likiwa ni kutaka kuendelea kufanya maboresho katika
utolewaji wa huduma hiyo.
Kwa mujibu wa ombi
Na,TR-W-15-008 kutoka
Muwsa kwenda Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji(EWURA) Mamlaka ya
maji safi na maji taka mjini Moshi
imetaka kuongeza beo ya huduma zake kwa mwaka 2015/2016 HADI
2017/2018.
Mabadiliko ya bei
hiyo inayopendekezwa itawahusu
makundi mbalimbali ya watumiaji wa huduma hiyo hususani wale wa
majumbani,Taasisi,Biashara ,Viwanda na wale wa kwenye
Vioski.
Mapendekezo mapya
ya bei ya utolewaji wa
huduma hiyo kutoka kiasi cha sh 495 kwa
Uniti moja ya ujazo wa maji ilivyo sasa hadi kufikia 710 katika kipindi
cha mwaka 2015/2016 na kiasi cha sh 746
kipindi cha mwa 2016/2017 kwa wateja wa majumbani na
taasisi.
Kwa upande wa
Biashara ,Muwsa imependekeza
bei ya huduma hiyo kuwa ni kiasi cha sh
839 kwa uniti moja kipindi cha 2015/2016,n ash 881 kipindi cha mwak
2016/2017 kutoka kiasi cha sh 585 katika ,kipindi cha mwa
2014/2015.
Eneo jingine ni kwa
watumiaji wa viwandani
,ambao Muwsa imepndekeza bei ya huduma kuwa ni kiasi cha sh 947 katika kipindi
cha mwaka 2015/2016 hadi kufikia kiasi cha sh 994 mwaka 2016/2017 kutoka 660 za
sasa.
Nao wamiliki wa
vioski bei iliyopendekezwa ni kiasi cha sh 696
katika kipindi cha mwa 2015/2016 hadi kufikia 731 katika kipindi cha mwala
2016/2017 kutoka kiasi cha sh 485 bei ya sasa.
Kutokana na hali
hiyo mamlaka ya udhibiti
wa wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeandaa mkutano na wananchi wa
manispaa ya Moshi ili kutoa maoni yao juu ya ongezeko la bei za huduma za maji
.
Mkutano huo
unatarajia kufanyika June 4
mwaka huu ,kuanzia majira ya saa 4 asubuhi , katika ukumbi wa Hindu Mandal
uliopo jirani kabisa na kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani cha mjini
Moshi.
Mgeni rasmi katika
mkutano huo anatazamiwa
kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama.
0 Comments