Basi
la Ngorika lenye namba za Usajili T770 BKW lililokuwa kitoka jijini Dar es
Salaam kwenda Arusha na lile la Kampuni ya RATCO T 274 DCP Tanga kwenda
Dar es Salaam yamegongana uso kwa huso na kulihusisha gari lingine dogo aina ya
Toyota Pass T 628 CXE na kusababisha vifo vya abiria 10 na majeruhi.
Ajali hiyo ilitokea eneo la Mbweni Mkata, wilayani Handeni mkoni Tanga.
Inaelezwa kuwa basi
la Ratco lilgongana kwanza na gari dogo na kisha kwenda kugongana uso kwa uso
na basi la Ngorika ambapo abiria 8 walifariki katika basi hilo na wawili
waliokufa walikuwa katika gari dogo wakipeleka mgonjwa hospitali.
Wakati
huo huo habari kutoka Morogoro zinaarifu kuwa Basi mali ya kampuni ya Happy
Nation lililokuwa likitokea jijini Dar es Salaam kwenda Mbeya limepata ajali
eneo la Kikwaraza Mikumi na kuuwa watu wawili na kusababisha majeraha kwa
abiria wengine 48.
|
0 Comments