Pambano la ngumi linalosubiriwa kwa hamu
Bingwa kulamba Euro mil 160
Pambano kupigwa Mei 2
LOS VEGAS, Marekani
MCHEZO wa ngumi ni kati ya michezo ambayo inapendwa
sana ulimwenguni kutokana na kuwa uhalisia
kwa kiasi kikubwa.
Ni mchezo wa hatari ambao umeshawapa vilema vya
baadhi ya viungo wachezaji wa mchezo huo kutokana na kutokuwa makini.
Kwa sasa pambano ambalo ndio limekuwa gumzo kwa mashabiki
wa ngumi ulimwenguni, ni kati ya Floyd Mayweather, Jr dhidi ya Manny Paquiao.
Pambano hilo na uzito wa middle linatarajiwa
kufanyika Mei 2 mwaka huu katika Ukumbi wa MGM Grand ndani ya Los Vegas.
Kwa kiasi kikubwa mashabiki wa mchezo wa ngumi
wanalisubiria kwa hamu pambano hilo kutokana na rekodi zilizopo kati ya mabondia
hao.
Ukiangalia kwa upande wa Mayweather ameshapigana
mapambano 47 na kushinda yote na kati ya hayo 26 ameshinda kwa KO.
Kwa upande wa Paquiano, ameshacheza mapambano 64 na
kushinda 57, K) 38 ambapo amepoteza matano na kutoa sare mawili.
Katika pambano la mwaka huu, lilianza kuadaliwa
tangu mwezi Januari baada ya masupastaa hao kukutana kwenye mchezo wa mpira wa
kikapu Miami na kuamua kukaa pembeni kwa ajili ya kuongelea mpambano huo mkali.
Baadaye walikubaliana kwa kubalilishana namba za
simu ambapo pia baadaye ilifahamika kuwa wamefikia muafaka.
Pamoja na kuwa walifikia muafaka lakini awali
Mayweather hakuwa tayari kulizungumzia pambano hilo kutokana na kuamua kuweka
siri, lakini baadaye ilibainika kuwa wameshainishana na kupanga siku ya pambano
ambapo waliamua kuanza kuitangaza katika vyombo mbalimbali vya Habari.
Pambano hilo ambalo ndilo litakalokata ngebe za
mabondia hao linatarajiwa kuhudhuriwa na umati wa mashabiki ambapo mpaka sasa
tiketi zimeshaanza kuuzwa.
Pambano hilo limegubikwa na utata ambapo awali
walikuwa wazipige mabondia hao lakini pambano liliahirishwa baada ya Pacquiao
kukataa kupima matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu.
Hata hivyo kwa sasa Pacquiao ametamka mwenyewe kuwa
anatarajia kumlipa faini ya pauni milioni 3.2 kwa Mayweather kama yeye
atashindwa kufaulu katika kipimo hicho safari hii.
Mkataba waliongia kati ya mabondia hao ni pamoja na
bingwa kuondoka na dau la Euro milioni 160.
Hata hivyo kwa sasa kumekuwa na tambo za hapa na
pale kwa mabondia hao kwa kila mtu kudai kuwa atafanya vizuri, lakini cha
msingi ni kusubiria Februari 2 kwa ajili kuona uhondo.
0 Comments