KOCHA SUPER D AMPIGA TAFU YA VIFAA BONDIA MUSSA CHITEPETE WA SONGEA VIFAA

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akimkabidhi vifaa bondia Mussa Chitepete wa Songea vilivyotolewa na Super D kwa kushilikiana na marafiki zake wa kwenye mtandao wengine kulia ni Kiliani Shayo na Rajabu Mkamba ambaye ni mdau mkubwa wa kuhamasisha kusaidia mchezo wa masumbwi Picha na SUPER D BOXING  .


Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akimkabidhi vifaa bondia Mussa Chitepete wa Songea vilivyotolewa na Super D kwa kushilikiana na marafiki zake wa kwenye mtandao wengine kulia ni Kiliani Shayo na Rajabu Mkamba ambaye ni mdau mkubwa wa kuhamasisha kusaidia mchezo wa masumbwi Picha na SUPER D BOXING 


Na Mwandishi Wetu
KOCHA wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kwa kushilikiana na marafiki zake wa kwenye mtandao wa kijamii wa watsupp wamemkabidhi vifaa bondia Mussa Chitepete wa Songea kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa masumwi nchini
Super D alimkabidhi vifaa hivyo bondia huyo hivi karibuni alivyotembelea jijini Dar es salaam kuja kushiliki mchezo wa masumbwi ambapo alipatiwa glove,gum shit,clip bandeji pamoja na kamba kwa ajili ya kurukia
vifaa hivyo vilivyotolewa na super D kwa kushilikiana na mdau mkubwa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mkumba ambaye ndie mwamasishaji mkubwa katika mtandao huo kwa ajili ya kusaidia mabondia
baada ya kukabidhiwa msaada huo bondia Mussa Chitepete wa Songea alishukulu wadau 
 mbalimbali kwa kumpatia vifaa na kumpongeza kocha Super D kwa kuanzisha mtandao ambaoumekuwa muhimu sana kwangu kwa mimi kupata vifaa najua sitotumia peke yangu wapo na wenzangu tutakao tumia nao pamoja vifaa hivi ambavyo itakuwa chachu ya kuinua mchezo wa masumbwi Songea

nae mdau mkubwa wa masumbwi nchini Rajabu Mkamba amesema kwa kushilikiana na Super D wamefanya mambo mengi kwa ajili ya kuinua mchezo wa masumbwi nchini hivyo atutoishia hapa tutaendelea kutoa sapoti kwa mabondia na wadau mbalimbali ili mchezo usonge mbele na wadhamini wajitokeze kusaidia ili vijana wawe na moyo wa kucheza mchezo wa masumbwi

Post a Comment

0 Comments