Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa kwaya ya Family Singers Jonas Danny akifafanua jambo katika mkutano na wandishi wa habari hawapo pichani wakati wakizungumza nao katika mkutano kuhusu uzinduzi wa DVD ya usilie itakayozinduliwa Desemba 7 mwaka huu katika ukumbi wa PTA Dar es Salaam anayefuata ni Daniel Misheto kutoka Misheto Promotion.
Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam
WAZIRI MKUU
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda ametajwa kuwa mgeni rasmi
kwenye uzinduzi wa albamu
‘Usilie’ ambayo itapatikana kwenye DVD Desemba 7 mwaka huu.
Akizungumza
jana kwenye mkutano na waandishi wa habari Mkurugenzi wa kwaya ya ‘Family
Singers’ Danny Misheto alisema kwamba
hafla hiyo itafanyika kwenye uwanja wa Sabasaba ulioko barabara ya Kilwa Jijini
Dar es Salaam.
Mbali ya
uzinduzi huo pia wasanii mbalimbali wa filamu watanogesha siku hiyo.
Aidha
waimbaji wa injili ambao ni Leah Mudy ,AIC (T) Vijana Chang’ombe, Accasia
Singers, Papson Mastaki kutoka Kenya na Frank Hume kutoka Boston nchini
Marekani watatumbuiza.
Uzinduzi huu
umeratibiwa na Misheto Promotion ambapo
kabla ya uzinduzi huo kutafanyika huduma
za bure za kiafya na kitabibu kutoka kwa madaktari bingwa wa magonjwa
mbalimbali ambayo yamekuwa yakiikabili jamii.
Misheto
anayataja magonjwa hayo kuwa ni moyo, figo, kisukari na mengineyo ambapo huduma hiyo itatolewa na
madaktari bingwa nchini.
“Huduma hii
itaanza saa mbili asubuhi na itatolewa
bure , ikiwemo ushauri na kwa wale ambao wataweza kutibika watatibiwa ila ambao
watakuwa kesi zao zimekuwa ni kubwa zaidi watapewa ushauri wa bure wa kuendelea
na matibabu katika hospitali kubwa” na kiingilio ni bure alisema Misheto.
0 Comments