PROFESA ANNA TIBAIJUKA.
Na Projectus Ishengoma Lugumalila
MHESHIMIWA
Bi.Anna Tibaijuka (MB) Waziri wa Ardhi ni moja wa viongozi wachache sana wenye
ujasiri na kiongozi muwazi katika sakata zima la Tageta ESCROW, kwani
kiongozi huyu amekiri wazi kuwa amepokea fedha Billion 1.6 kutoka kwa mmiliki
wa Kampuni ya VIP Engineering Bw.James Rugemalira tena si fedha ndogo.
Si
jambo jema kumuhukumu Mheshimiwa Anna Tibaijuka lakini siyo vibaya kumshauri kwa
kuwa amekuwa muwazi katika sakata hili,basi lingekuwa jambo la maana sana kama
angejiuzulu madaraka aliyonayo katika serikali ili kulinda heshima yake na ya
chama tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Msomi
yoyote yule anapofikia kuitwa Profesa na tena Waziri mwenye kushika dhamana
ya nchi na wananchi yaani Ardhi na makazi, ardhi ndio kila kitu kwa
Watanzania, halafu
akafikia sehemu ya kukubali kupokea fedha ya kiasi kikubwa Sh. Billion 1.6 kutoka kwa mfanyibiashara ! naye Mhe.Anna Tibaijuka bila ya kutia
shaka yoyote kama ananunuliwa kwa namna moja au nyingine kutokana na
dhamana ya cheo chake? hapa kwa Mtanzania yoyote haingii akilini.
Litakuwa
jambo bora kwa Mhe.Anna Tibaijuka kujiuzulu ili aonyeshe mfano bora kuwa
yeye ni Kiongozi mkweli na Viongozi wengine watafuata nyayo.
Tunajua
mtu anapoitwa Profesa siyo msomi wa kawaida bali msomi aliefikia daraja la
juu kabisa,ndiyo maana tunaona msomi kama kiongozi wetu huyu ambaye anajua wazi
kuwa yeye ni mmojawapo wa Mawaziri wachache ambao Wizara zao
zina
dhamana kubwa ya nchi, leo hii anakubali kununuliwa kiurahisi pia kufanya
biashara akiwa katika madaraka mazito,kama ataendelea kututumikia wananchi katika Wizara ambayo pia inahusika na mipaka ya ardhi ya nchi,tuna mashaka nae.
Watanzania
tunajiuliza hivi Tibaijuka yupo katika utumishi wa umma tena katika Wizara muhimu na huku akiwa Mkurugenzi wa Mashirika au shule na miradi binafsi
au? ndiyo kusema cheo chake cha utumishi wa umma ndio dhamana
ya biashara zake ?
Hivi
kuna hosptali ngapi hapa nchini hazina dawa? je wakina mama wangapi wajawazito
wanafariki wakati wa kujifungua kwa ukosefu wa vifaa vya mahosptalini? Shule
ngapi ? za serikali ambazo hazina madawati?
Leo
Mheshimiwa ambaye tena ni Profa amepokea fedha Sh.Billion 1.6 na
kusema kuwa hakujua kama ni fedha chafu, watanzania tunamashaka nae.
"Profesa Tibaijuka anafahamu wazi kuwa amevunja sheria ya maadili ya viongozi
wa umma
(Sheria namba13 ya mwaka 1995) ambayo inawataka viongozi watoe
taarifa ya zawadi wanazopokea au malipo wanayolipwa".
Sisi
wananchi wenye kuiamini serikali hii na juhudi za Kiongozi wetu Mhe.Rais
Dkt. Jakaya Kikwete (Mungu amuongezee afya njema), hatuwezi kabisa
kukubali au kuona kiongozi tena msomi Profesa ,anavunja dhamana ya
wananchi na kumvunjia heshima mkuu wa nchi ambaye ndiye alikuteuwa.
Litakuwa
jambo la busara sana Tibaijuka ujiuzulu ili kulinda heshima yako
kama msomi Profesa ,pia kulinda heshima serikali na chama tawala.
Huwezi
kutumikia ofisi mbili utumishi wa umma na biashara. Wanachi
tunasikitika sana kuona katika sakata la fedha za umma mpaka baadhi ya watumishi wa mungu ambao ni viongozi wa Kanisa nao wanahusika na
bila ya uwoga wanapokea fedha bila ya hofu ya kujenga udini.
Mungu
ibariki Tanzania,Mungu mzidishie afya njema kiongozi wetu Raisi Kikwete .
0 Comments