Waamuzi
23 wa daraja la kwanza wakiwemo wenye beji la Shirikisho la Kimataifa
la Mpira wa Miguu (FIFA) wameteuliwa kushiriki semina itakayofanyika
Novemba 16 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Washiriki
wa semina hiyo ambayo pia itakuwa na mtihani wa utimamu wa mwili
(physical fitness test) wanatakiwa kuripoti Novemba 15 mwaka huu kwenye
hosteli ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyopo Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume.
Wakufunzi wa semina hiyo wanaotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ni Riziki Majala na Soud Abdi.
Waamuzi
watakaoshiriki semina hiyo ni Ahmed Juma Simba (Kagera), Arnold Bugado
(Singida), Charles Peter Simon (Dodoma), Dalila Jafari Mtwana
(Zanzibar), Ferdinand Chacha Baringenge (Mwanza), Florentina Zabron
(Dodoma) na Frank John Komba (Pwani).
Grace
Wamara (Kagera), Hellen Joseph Mduma (Dar es Salaam), Israel Mujuni
Nkongo (Dar es Salaam), Issa Bilali Ali (Zanzibar), Issa Haji Vuai
(Zanzibar), John Longido Kanyenye (Mbeya), Jonesia Rukyaa Kabakama
(Kagera) na Josephat Deu Bulali (Tanga).
Kudra
Omary (Tanga), Martin Eliphas Saanya (Morogoro), Mary Kapinga (Ruvuma),
Mfaume Ali Nassoro (Zanzibar), Mgaza Ali Kinduli (Zanzibar), Samwel
Hudson Mpenzu (Arusha), Soud Iddi Lila (Dar es Salaam) na Waziri Sheha
Waziri (Zanzibar).
0 Comments