UONGOZI wa Kampuni ya The African Stars Entertainment wanaomiliki bendi ya Thwanga Pepeta wameandaa onyesho maalum la madhimisho ya miaka 16 ya mwanamuziki wake gwiji wa kike Luiza Mbutu.
Akizungumza na Bongoweekend Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Asha Baraka alisema kua wameandaa onyesho hilo ambalo litakua maalum kwa kuenzi na kiuthamini mchango wa Kiongozi wa bendi hiyo ambaye anatimiza miaka 16 ndani ya bendi bila kuhama tangu ilipoanzishwa.
“Uongozi wa
ASET umeamua kuandaa usiku maalum wa kumuenzi Luiza kutokana na kua na
msimamamo wa kukaa katika bendi kwa muda wote huo bila kuhama hilo ni jambo la
kujivunia” alisema Asha.
Aliongeza
kwa kusema kuwa onyesho hilo litakwenda kwa jina la Luiza Mbutu na Twanga
Pepeta ambalo pia kutakuwa na shamrashamra zake ambazo zitatajwa siku
itakapowadia” alisema Asha.
Pia
aliongeza kwa kusema kuwa wao kama ASET wanatambua mchango wa Luiza ndani ya
bendi hiyo hivyo kutakuwa na tukio la aina yake ambalo mashabiki na wadau wa
bendi hiyo pamoja na wapenzi wa Luiza wajitokeze kwa wingi siku hiyo kushuhudia
litakalojiri sambamba na kupata burudani kutoka kwa bendi ya Twanga Pepeta.
Onyesho hilo
limepangwa kufanyika Desemba 6 mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Mango Garden Jijini
Dar es Salaam.
0 Comments