SHEREHE YA MIAKA 50 YA BENDI YA MSONDO NGOMA "BABA YA MUZIKI" YAFANA




 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akimkabidhi Cheti cha heshima Kiongozi wa Bendi ya Msondo Ngoma,Mzee Said Mabera.
*******************************
Bendi Kongwe ya Muziki wa Dansi hapa nchini iliyodumu kwa miaka 50 toka kuanzishwa kwake mwaka 1964,Msondo Ngoma Music Band imesherehekea jubilei yake hiyo iliyofanyika Novemba 1,2014 katika viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha mashabiki wake lukuki kutoka sehemu mbali mbali.
 
Mgeni Rasmi katika Sherehe hizo za kusherehekea Jubilei ya miaka 50 ya Bendi ya Msondo Ngoma,alikuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel ambaye aliweza kuwatunuku vyeti vya heshima wanamuziki mbali mbali walioitumia Bendi hiyo toka ilipoanzishwa mpaka sasa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea Cheti cha heshima kutoka kwa Muwakilishi wa Mfuko wa PSPF,Abdul Njaidi ambao ni sehemu ya Wadhamini wa Bendi hiyo ikiwa ni sehemu ya heshima kwa Mh. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa mchango wake mkubwa kwa wasanii mbali mbali hapa nchini.Cheti hicho kimetolewa na Bendi ya Msondo Ngoma.Picha Zote na Othman Michuzi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akimkabidhi Cheti cha heshima mpiga solo hodari wa Bendi ya Msondo Ngoma,Abdul Ridhwan "Panga mawe"
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel akimkabidhi Cheti pamoja na fedha taslim sh. Laki 5,Mke wa Marehemu Mzee Muhidin Maalim Gurumo katika hafla hiyo ya kutimiza miaka 50 ya kuanziswa kwa Bendi hiyo.
Mmoja wa Waanzilishi wa Bendi hiyo,John Simon (Kapten Mstaafu) akizungumza machache pamoja na kutoa historia fupi ya kuanza kwa bendi hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akimkabidhi Cheti pamoja fedha taslim sh. Mil. 5,Hassan Moshi William (mtoto wa Marehemu TX Moshi Willian) kwa niaba ya baba yake.
Mtangazaji Mkongwe hapa nchini na mwenye historia na Muziki wa Tanzania,Masoud Masoud (kulia) akionyesha moja ya CD za bendi ya Msondo Ngoma zilizokuwa zikinadiwa kwenye sherehe hizo mbele ya Wadhamini.
Safu ya waimbaji wa Bendi ya Msondo Ngoma ikiongozwa na Nguli Shaaban Dede (katikati) wakifanya vitu vya mbele ya mashabiki wao lukuki waliofika kwenye Viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar.
Mpiga Tumba wa Msondo Ngoma akifanya yake.
Hassan Moshi William (mtoto wa Marehemu TX Moshi Willian) akionyesha uhodari wake kiasi kwamba hata pengo la mzee wake kuhisi limezibwa.
Rapa wa Bendi ya Msondo Ngoma,Roman Mng'ande akifanya mambo.
Baba la Mababa,Mzee Said Mabela akiendeendelea kuzikonga nyoyo za Mashabiki wa Msondo. Picha kwa hisani ya Othman Michuzi

Post a Comment

0 Comments