ALIYEKUA Redds
Miss Tanzania Sitti Abbas Mtemvu
ametamka rasmi kuvua taji hilo ambalo alilitwaa 0ktoba 11 mwaka huu kwenye
fainali za shindano zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.
Katika barua
iliyoandikwa na Sitti kwenda kwa Kamati ya Miss Tanzania Sitti alisema hivi: Sitti Abbas Mtemvu S.L.P 60 151 Dar es
Salaam 5.Novemba 2014.
Mkurugenzi
Lino International Agency Limited Dar es Salaam, Yah:Kuvua taji la Miss Tanzania 2014.
Ndugu
Mkurugenzi tafadhali husika na kichwa cha habari hapo juu, “Mimi Sitti
Abbas Mtemvu, baada ya kutwaa taji la urembo la Miss Tanzania mwaka 2014
kumezuka shutuma mbalimbali dhidi yangu .Wameniwekea maneno
mengi sana mdomoni kwamba nimesema wakati siyo”.
Shutuma
hizo zimeandikwa katika vyombo mbalimbali vya habari , Blogs
na Mitandao ya Kijamii, kiasi ambacho naona inaweza hata kuhatarisha
maisha yangu.
Sasa kwa hiari yangu mwenyewe tena
bila kushawishiwa na mtu
na kwa kulinda heshima yangu
pamoja na familia yangu
natamka rasmi kuvua taji la
urembo la Miss Tanzania 2014.
“Napenda niwashukuru
wale wote waliokuwa wakinipa sapoti tangu mwanzo nilipoingia katika
mashindano haya katika ngazi ya Taifa , nao ni warembo wote wa
Chang’ombe, Temeke, pamoja na wote
tuliokuwa nao katika fainali za Taifa.
Pia
napenda kutuma shukrani za dhati kwa Waandaaji wote wa kituo cha
Chang’ombe, Temeke na Wajumbe wa Kamati
ya Miss Tanzania kwa mafunzo mbalimbali
niliyoyapata.
Nawashukuru pia waandishi wa habari wote kwa mchango wenu ,
pamoja na Wizara ya Habari , Utamaduni
na Michezo na Baraza la Sanaa la Taifa kwa busara zenu.
Sitti
anamaliza kwa kusema “Leo nalivua rasmi
taji nililopewa na binadamu
lakini taji alilonipa Mweyeezi Mungu bado ninalo, mwisho naomba radhi Watanzania wote kwa uamuzi huu niliouchukua.
Naye Hashim
Lundenga akizungumza mbele ya waadishi
wa habari katika mkutano uliofanyika
kwenye hotel ya JB Belmont alisema kwamba wamepokea barua hiyo Novemba 6 na wana heshimu uamuzi wa Sitti.
“Tumepokea
barua ya Sitti hivyo nafasi yake itachukuliwa na aliyekuwa
shindi wa pili Lilian Kamazima ambaye ni Miss Arusha pia Miss Kanda ya
Kaskazini” alisema Lundenga.
Akijibu swali kuhusu zawadi ambazo ni kitita cha sh. Mil 18 , alisema hivi sasa ni
mapema mno kujibu suala hilo hivyo taratibu za kiofisi zitafuatwa na watatoa
tamko.
Kamazima
alisema kwamba anafurahia kupata nafasi hiyo ya kuwa Miss Tanzania hivyo ataanza kwa kujipanga na kufanya kazi
za kijamii ikiwa ni sehemu ya maandalizi yake ya kuiwakilisha nchi kwenye
shindano la kumtafuta mrembo wa dunia litakalofanyika mwakani.
0 Comments