Bondia Maisha Samson kushoto
wakitunishiana misuli na Ibrahimu Tamba wakati wa utambulisho wa
mpambano wao utakaofanyika jumapili ya novemba 9 katika ukumbi wa
manyara park tandale CCM Picha na SUPER D BLOG
Bondia Maisha Samson kushoto wakitunisha misuli na
Ibrahimu Tamba wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika
jumapili ya novemba 9 katika ukumbi wa manyara park tandale CCM Picha na
SUPER D BLOG
Samson Maisha
Ibrahimu Tamba
Mabondia Ibrahimu Tamba wa Dar kushoto na Samson Maisha wa Kyela
Mbeya wakinyoshwa mikono juu na mratibu wa mpambano huo Jafari Ndame wakati wa utambulisho wa mpambano wao
utakaofanyika Jumapili ya Novemba 9 katika ukumbi wa Manyara Park
Tandale CCM Picha na SUPER D BLOG
Mabondia Ibrahimu Tamba wa Dar na Samson Maisha wa Kyela
Mbeya wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao
utakaofanyika Jumapili ya Novemba 9 katika ukumbi wa Manyara Park
Tandale CCM katikati ni mratibu wa mpambano huo Jafari Ndame Picha na SUPER D BLOG
NGUMI KUPIGWA JUMAPILI MANZESE UKUMBA WA MANYARA
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Samsoni Maisha wa kyela
Mbeya amewasili jijini Dar es salaam na kutamba kunyakuwa ubingwa wa
TPBO kwa kumpiga Ibrahimu Tamba wakati wa mpambano utakaofanyika novemba 9 mwaka huu katika
ukumbi wa Manyara Park Manzese Dar es salaam
mpambano huo wa raundi kumi kugombania
ubingwa wa taifa unaotambuliwa na TPBO utatanguliwa na mpambano
mwingine wa ubingwa kati ya julius Kisarawe na
Moro Best mpambano wa raundi kumi pia
mwandaaji wa mpambano huo Jafari Ndame amesema maandalizi yote yapo
tayali hivyo wanasubili siku tu kukamilisha mpango mzima
aliongeza kuwa siku hiyo kutakuwa na
mapambano mengine ya utangulizi ambapo Karim Ramadhani atapambana na
Stevin Kobelo na Robinson Msimbe atamenyana na Fadhili Boika na
mipambano mingene mikali zaidi siku hiyo kutakuwa na michezo ya
utangulizi zaidi ya nane yenye raundi sita sita
0 Comments