REDBULL WAMLETA BINGWA WA KUPIGA MISELE NA PIKIPIKI KUTOKA AFRIKA KUSINI

MWANAMICHEZO ambaye anacheza kwa kutumia chombo cha moto Pikipiki  Bryan Capper yuko nchini kwa mwaliko maalum akitoka nchini kwao Afrika kusini ametoa wito kwa watanzania kucheza mchezo huo ambao mbali ya kufurahisha pia unatumia akili na kukufanya uwe mkakamavu wakati wote.

Akizungumza leo asubuhi  katika viwanja vya Coco Beach  Jijini Dar es Salaam ambako ndiko alikoanza kuonesha onyesho lake la kwanza  na kuonesha umahiri wake katika uendeshaji wa pikipiki  yupo nchini kwa kudhaminiwa na Kampuni ya Red Bull, atakuwa nchini kwa ziara ya  siku tatu.

Kesho  Jumapili atakuwa katika viwanja vya Mlimani City na  Jumatatu atahitimisha ziara yake katika eneo la Ubungo Tanesco.

Capper amesema kwamba amefurahia kuweza kufika nchini Tanzania  pia tayari ameshafanya maonyesho yake katika nchi za Kenya na Uganda.

Wakati huohuo Rais wa Tanzania Motorcross Acrobatic Club , Blagina Mwihava alisema kwamba wamemleta  mwanamuchezo huyo ambaye wana imani kubwa ataleta msisimko mkubwa kwa vijana wa kitanzania kuweza kupata hamasa ya kucheza mchezo huo wenye mvuto.    

 “Hii itakuwa ni shoo kwa watanzania  ili waweze kuvutika kucheza mcheo huu wa aina yake .

Ziara ya mchezaji huyo imeratibiwa na Kampuni ya Mohans  inayosambaza kinywaji cha Redbull nchini maonesho hayo yote  ni ya wazi.

Post a Comment

0 Comments