Aidha bendi hiyo inatarajiwa kufanya ziara ya kimuziki katika mikoa ya Morogoro na Dodoma wiki ijayo kwa ajili ya kuzitambulisha nyimbo zao mpya za albamu hiyo kwa mashabiki wa mikoa hiyo.
Msemaji Msaidizi wa Sikinde, Emmanuel Ndege aliiambia MICHARAZO kuwa baada ya kukwama kufanya uzinduzi wao Agosti kama ilivyokuwa imetangazwa, Sikinde sasa inatarajiwa kuzindua albamu yao mpya katika maadhimisho ya miaka 38 ya kuanzishwa kwa bendi hiyo.
Ndege alisema kwa sasa wanaendelea kufanya mchakato wa wadhamini kabla ya kutangaza rasmi tarehe ya jambo hilo, japo alisisitiza itakuwa mwishoni mwa Oktoba.
"Uzinduzi wa albamu yetu mpya utafanyika Oktoba sambamba na maadhimisho ya miaka 38 tangu kuanzishwa kwa Sikinde," alisema Ndege.
Pia aligusia juu ya ziara ya kimuziki wanaotarajia kuifanya wiki ijayo katika mikoa ya Morogoro na Dodoma ili kutambulisha nyimbo zao mpya kwa mashabiki wa bendi hiyo wa mikoa husika.
"Tupo katika maandalizi ya kwenda kuzitambulisha nyimbo za albamu yetu mpya katika mikoa ya Dodoma na Morogoro, tukiwa huko pia tutakumbushia nyimbo za zamani za bendi hiyo zilizoipa Ubingwa wa Muziki wa Dansi Tanzania," alisema Ndege
0 Comments